Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Dar es salaam Janeth Elias Mahawanga amekutana na vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha Jimbo la Ukonga Mkoani humo ikiwa ni kutimiza majukumu yake akiwa kama mwakilishi wa vikundi hivyo katika Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbunge huyo amesema pia amekutana na vikundi hivyo kwa mambo matatu ambayo ni kushiriki nao miradi ya maendeleo, kutoa mrejesho wa Bunge la Bajeti na kupokea changamoto mbalimbali sambamba na kurudisha majibu ya baadhi ya mambo ambayo aliwatuma kuwauliza Bungeni na kuhakikisha anapaza sauti zao na kufuatia mkutano wa Ras Samia Suluhu Hassan na wanawake wa Tanzania uliofanyika uliofanyika Jijini Dodoma mwezi wa na sita mwaka huu.
Mbunge huyo ameviomba vikundi hivyo kutizama ipasavyo fursa ambazo Rais Samia amezianzisha ili kuimarisha uchumi wao. Vilevile amesema amebahatika kupata wadau ambao wapo tayari kushirikiana na wajasiriamali ambao wamekata tamaa kabisa KWa kukosa motaji na kuwa kwenye foleni kwa muda mrefu kusubiri mikopo.
"Mwezi wa kumi tutaanza project ya "Mwanamke wa Dar ea salaam Tisha Mama, kwa nini usiwe wewe" kwa kupata bidhaa moja kwa moja kutoka kiwandani bila kuwa na mtaji wowote ambayo itafanyika chini ya Taasisi ya TISHA MAMA FOUNDATION. Mimi ninaanini penye Maendeleo ya Mkoa wetu yataletwa na sisi wenyewe" alisema Mbunge huyo Janeth Mahawanga.
Mahawaga aliwaSa wanavikundi hao kupendana na kushirikiana mana bila kufanya hivyo hawataweza kusonga mbele na kila watakapomuhitaji wasisite kumuita kwani yeye yupo na atawafata huko huko walipo.
Home
HABARI
MBUNGE VITI MAALUM MKOA WA DAR ES SALAAM AKUTANA NA WAJASIRIAMALI WA VIKUNDI VYA KIJAMII VYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...