Na Abel Paul-Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.John Mongela amewataka wananchi wa Mkoa wa Arusha kuachana na mikusanyiko isiyo ya halali na kutumia barakoa kunawa maji tililika kujikinga na ugonjwa wa korona, ambao unasumbua dunia katika kipindi hiki.
Ametoa kauli hiyo jana Julai 22/2021 katika ziara yake na wadau wa kilimo cha matunda, mboga mboga, na kilimo cha maua(TAHA) katika wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.
Kwa upanda wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP-JUSTINE MASEJO amesema "Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limepokea maelekezo hayo ya serikali ngazi ya Mkoa kwa wale wote watakao fanya mikusanyiko isiyo halali, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...