MCHEZAJI wa timu ya Taifa ya Tanzania Twiga Stars na klabu ya JKT Queens Stumai Abdallah Athuman (Kuchini) amekuwa mchezaji wa kwanza wa soka la wanawake Tanzania kusaini mkataba na kampuni ya Jeff Sports Management ambayo itakuwa inasimamia mambo yake ya soka na biashara.
Jeff wameingia mkataba na Stumai ambao hawajaweka wazi ni wa muda gani wa kumtafutia masoko ya kisoka na biashara, ambapo watakuwa wanahusika kumtafutia timu ndani na nje na nchi lakini kubwa zaidi kumtengeneza mchezaji kuwa biashara kupitia bidhaa mbalimbali ambazo zitakuwa na nembo ya jina lake.
Jeff watatumia jina lake la utani la Kuchini ambalo wamelifupisha hadi kuwa Kuchi, kisha watachukua namba nane ambayo ni namba ya muda mrefu kwenye jezi zake na kuwa Kuchi8, ambayo ndiyo itakuwa jina litakalotangaza bidhaa zake mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuzindua wa nembo hiyo na kumtambulisha mchezaji huyo, kwenye hoteli ya Atriums iliyopo Sinza Dar, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo John Lyadumda alisema wamemchukua Stumai kwa kuwa ni mtu sahihi na amekuwa na muonekano wa kike na nidhamu Superb ambavyo ni vigezo vikuu vya kampuni hiyo.
Kwenye uzinduzi huo Jeff walitambulisha T-shirt zenye nembo ya Kuchi8 ambazo zitapatikana nchi nzima, lakini pia kutakuwa na vikombe, Key Holders, mgauni, sandals na bidhaa nyingine za kike. Jeff walimkabidhi pia vifaa binafsi vya mazoezi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...