Na Linda Shebby
MAMIA ya wakaazi wa Mkoa wa Dar Es Salaam leo walihudhuria tamasha lililofana ambalo lilikwenda kwa jina la 'Mihogo Festival' lililofanyika kwenye ufukwe wa Coco, maarufu kwa jina la 'Coco Beach' ambako kumesheheni wachuuzi wa mihogo ya kukaanga na mishikaki.
Akizungumza na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Ubunifu kutoka Clouds Media Group (CMG) Sebastian Ndege amesema imekuwa ni kawaida kwao kuwa wabunifu kwa kuleta michongo kwa jamii ikiwa ni katika kupandisha thamani ya kitu chochote Kama jinsi walivyoipandisha thaamani mihogo chakula ambacho wapo baadhi ya watu ambao wamekua wakiushusha thamani muhogo huku zao hili likiwa ni lenye thamani ulimwenguni.
"Ifike wakati sisi Watanzania tujivunie asili yeti kama jinsi ambavyo mtu unaweza kwenda katika nchi za wenzetu Kama Italy wao wana tamasha lao la Pizza Festival vivyo hivyo na sisi tumekuja na tamasha hili la Muhogo Festival" Alisema Ndege.
Aidha tamasha Hilo lilinogeshwa na wasanii mbalimbali akiwemo msanii Mkongwe katika muziki wa dansi Muumin Mwinjuma,Malaika, Bosho,Ferouz,Rich Mavoko,Kayumba,Fay Melody,Ney Wamitego, Msami,Sarafina,,Young D,Frida Amani, Country Boy,DJ ODG,Dulla Makabila na Sholo Mwamba.
Aidha Ndege aliongeza kwa kusema kuwa chachu ya kufanyika kwa tamasha hilo ilitoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group (CMG) Joseph Kusaga ambaye ni mteja mkubwa wa wachuuzi hao wa mihogo ambapo waliwahi kumuuliza mbali ya kuwa yeye ni mteja wao mkubwa wa mihogo atawafanyia nini ambapo aliwaahidi kuwaandalia tamasha hivyo ametimiza ahadi yake, Alisema.
Aliongeza kwa kusema kuwa CMG wamekua wakipandisha thamani bidhaa mbalimbali ikiwemo mtu mmojammoja ama vikundi, Kama Tasnia za urembo, michezo Ndondo Cup, Malkia wa Nguvu, na wasanii katika nyanja zote.
Watangazaji wa Clouds Tv Dacota Delavida na Sakina Lyoka wakiwa Jukwaani kwenye tamasha la Mihogo Festival lililofanyika kwenye Ufukwe wa bahari ya Hindi almaarufu Kama.Coco Beach Jijini Dar Es Salaam
MC Konata anyetamba na miondoko ya Singeli akitoa burudani kwenye tamasha la Mihogo Festival lililofanyika kwenye Ufukwe wa bahari ya Hindi almaarufu Kama.Coco Beach Jijini Dar Es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...