Na Said Mwishehe, Michuzi TV
WATANZANIA wanaotembelea Maonesho ya 45 Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu Sabasaba,Dar es Salaam wameshauriwa kutembelea banda la East -West Seed Tanzania kwa ajili ya kupata mbegu bora za matunda na mbogamboga.

Ushauri huo umetolewa na Msanii maarufu nchini Mrisho Mpoto ambaye ni Balozi wa East-West Seed Tanzania alipotembelea banda hilo kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ubora wa mbegu za matunda na mbogamboga ambazo zinauzwa na kusambazwa na East -West Seed Tanzania.

"Nimekuja banda la East-West Seed kwa kuwa mimi ni balozi wao na nimekuwa nikitangaza bidhaa zao ambazo ni mbegu bora za matunda na mbogamboga, naomba niwashauri wananchi wanaokuja kwenye maonesho haya kufika kwenye banda hili.

"Wakiwa hapa mbali ya kuona matunda ambayo tumekuja nayo kwa ajili ya kuowanesha watanzania, wataona aina mbalimbali za mbegu na sio tu kuona bali wataelezwa kwa kina kuhusu mbegu zetu na ubora wake.Sote tunafahamu mbegu ni kitu muhimu sana kwani hata unapoangalia changamoto nyingi zinazowakabili wakulima mojawapo huwa linaanzia kwenye mbegu,"amesema Mpoto.

Amefafanua wakulima walio wengi wanataka kuona matokeo lakini wanasahau mbegu ndio msingi wa kilimo chenye kutoa mazao bora na yenye tija."Kwa hiyo East-West Seed tumejikita katika mbegu tu na jukumu letu ni kuuza na kusambaza mbegu za mboga mboga na matunda.

"Ndio maana katika maonesho haya East-West Seed wamekuja kuonesha matunda na hapa tumekuja na mbegu mbalimbali, tumekuja na mbegu ya nyanya inayofahamika Imara F1 ambayo hii ina uwezo wa kukaa siku 31 bila kuharibika, ina uwezo mkubwa wa kuvumilia magonjwa, na mavuna kwa mmea mmoja ni kati ya kilo tano hadi kilo 10.Pia tunayo mbegu ya nyanya ya Kipato F1,Rio Grande VF Improved.

"Tunayo mbegu ya Yolo Wonder Improved(Hoho) ambayo hukomaa baada ya siku 70 mpaka 75, na kiasi cha mbegu kwa ekari moja ni gramu 100 na mavuno yake ni tani 15 hadi tani 20 kwa ekari.Kwa ujumla tunazo mbegu za matunda na mbogamboga za akila aina, ukija East-West Seed utaona matikiti ambayo tumekuja kuwaonesha wananchi jinsi yalivyokuwa makubwa.

"Tumekuja na mapapai, bilinganya, nyanya chungu, bamia ili anayekuja aweze kuona kwa macho yake kile ambacho tunamueleza,"amesema Mpoto na kusisitiza "Ukiangalia mbegu za tikiti la Mkombozi utaliona ni kubwa na bora ukilinganisha na matitiki yanayotokana na mbegu nyingine.

"Watu wengi wanalima tikiti lakini kwa bahati mbaya wanapata mbegu ambazo zimechakachuliwa na hazina ubora lakini East -West Seed tunauza na kusambaza mbegu bora , hata ukiangalia kauli mbiu yetu tunasema mbegu bora kwa mapato mazuri."
Msanii Mrisho Mpoto'Mjomba Mpoto'(kulia) ambaye ni Balozi wa East-West Seed Tanzania(EWTZ) akizungumza na baadhi ya maofisa wa kampuni hiyo baada ya kutembelea banda lao lililopo kwenye Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu Sabasaba mkoani Dar es Salaam.Mpoto ni balozi wa East-West Seed Tanzania.
Msanii Mrisho Mpoto (kulia) akizungumza na baadhi ya maofisa wa East-West Seed Tanzania alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali yaliyomo kwenye Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu Sabasaba.
Mrisho Mpoto(kulia) akiwa ameshika kipeperushi cha East-West Seed Tanzania wakati akielezea ubora wa mbegu zinazozalishwa na kampuni hiyo baada ya kutembelea banda lao lililopo Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa.Mpoto ni balozi wa kampuni hiyo ambayo inajihusisha na uzaaji na usambazaji wa mbegu za mbogamboga na matunda.
Wasanii wa ngoma za asili na sarakasi wakitoa burudani kwa wananchi walioko kwenye Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu Sabasaba mkoani Dar es Salaam.Wasanii hao walikuwa wameongozana na Mrisho Mpoto alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbal yaliyomo kwenye maonesho hayo likiwemo banda la East-West Seed Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...