Leo Julai 19,2021 Naibu Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Dkt. Kathrin Steinbrenner amemtunuku Dkt. Karl-Heinz Köhler tuzo ya the order of Merit Cross on Ribbon ya Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani katika makazi ya Balozi.
Taarifa iliyotolewa leo na Kitengo cha Mawasiliano cha Ubalozi huo imesema kuwa Mwishoni mwa mwaka 2010, Dkt. Karl-Heinz Köhler pamoja na Mratibu wa Shirikisho wa miradi ya shule za UNESCO Ujerumani, Heinz-Jürgen Rickert na Mratibu wa Kitaifa wa mtandao wa shule za UNESCO nchini Tanzania, Modester M.Mwinula, walianzisha “Tasisi ya ujifunzaji wa utamaduni na ubunifu /Shule za mfano za Afrika”
Ambapo kwa kipindi chote Dkt. Köhler amekuwa ni Mkurugenzi Mkuu.”Shule ya Sekondari Dunia Moja Kilimanjaro” iliyoanzishwa mwaka 2012 kama mradi wa jaribio na ilikuwa mradi wa shule ya Unesco ya kwanza nchini Tanzania yenye mwelekeo wa kimataifa.
Imesema kwamba Shule ya Sekondari ya Dunia Moja Kilimanjaro iliyopo Kisangara ,takriban km 60 kusini mwa Moshi na mkoa wa Kilimanjaro, inaunganisha mifumo ya shule za Ujerumani na Tanzania, mbinu za kujifunza za kijerumani na pia wanafunzi wanajifunza Kijerumani kama lugha ya pili ya kigeni baada ya Kingereza. Shule imesimama katika mtindo wa kisasa wa elimu inayosaidia watoto wa Kitanzania na vijana kuwa na maisha ya kujitegemea.
Kutokana na jitihada za Dkt. Köhler “Shule ya Sekondari Dunia Moja Kilimanjaro” kwa sasa ni mojawapo ya shule tatu za PASCH nchini Tanzania.PASCH inawakilisha “Shule: Washirika wa siku zijjazo” mpango wa kijerumani iliyozinduliwa Februari mwaka 2008 na ofisi ya Shirikisho ya Mambo ya Nje ya Ujerumani lenye lengo la kuamsha hamu na shauku kwa vijana kujifunza Kijerumani na kutengeneza mtandao wa kimatifa wa shule ambapo mpaka sasa inajumuisha shule 200 duniani kote.
Dkt. Köhler ametoa mchango mkubwa kwa sifa ya Ujerumani katika nyanja ya elimu.
Home
HABARI
NAIBU BALOZI WA UJERUMANI NCHINI TANZANIA KWA NIABA YA JAMHURI YA SHIRIKISHO LA UJERUMANI AMEMTUNUKU DKT.KARL-HEINZ KÖHLER TUZO YA THE ORDER OF MERIT CROSS ON RIBBON
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...