Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi leo amefanya ziara kwenye mitambo ya uzalishaji Maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini ili kuona ufanisi wa miradi hiyo ya maji ya DAWASA.
Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara Mhandisi Mahundi amesema kuwa Serikali imeshaanza kusambaza Mita za maji za kulipia kadri ya matumizi husika yaani Pre Paid Meter ili kuondoa Changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na bili bambikizi.
Mhandisi Mahundi amesema kuwa wamefika hatua ya kuanza matumizi ya mita hizo kufuatia malalamiko ya Wananchi ambao wanadai kuwa wanabambikiziwa Bili kubwa kuliko matumizi yao jambo ambalo ni kinyume na inavyotakiwa.
Mahundi amesema kuwa watahakikisha ifikapo 2025 upatikanaji wa maji safi katika maeneo ya mijini unafikia asilimia 95 huku Vijijini ikifika asilimia 85.
Pia Mhandisi Mahundi ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) chini ya Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja kwa kuendelea kutoa huduma ya maji pamoja na utandikaji wa mabomba sehemu zote ambazo maji hajafika maana kufanya hivyo wanapunguza tatizo la upatikanaji wa maji kwa wananchi.
Naye Mkurugenzi wa Uzalishaji Na Usambazaji Maji Dawasa Shaban Mkwanywe ametolea ufafanuzi maeneo ambayo yanahudumiwa na Mtambo wa Ruvu Chini pamoja Ruvu Chini na namna walivyojipanga kuwafikishia wananchi huduma ya maji kwenye Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Huu ni mwendelezo wa wa serikali kuhakikisha inaondoa Changamoto Ya Upatikanaji wa Maji Katika Maeneo mbalimbali Nchini. Hivyo DAWASA wamejipanga kuweza kumaliza changamoto ya maji kwa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Mkurugenzi
wa Uzalishaji na Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa
Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Shabani Mkwanywe
akimkaribisha pamoja na kumpa utangulizi Naibu Waziri wa Maji, Mhe.
Mhandisi Maryprisca Mahundi(wa kwanza kushoto) kuhusu Mtambo wa Ruvu Juu
unavyofanya kazi wakati wa Ziara ya Naibu waziri alipotembelea Mtambo
huo pamoja na kujionea ufanyaji kazi wake.
Meneja
wa Mtambo wa Ruvu Juu Mhandisi Edward Mkilanya akitoa ufafanuzi kwa
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi(wa pili kulia)
kuhusu mchakato wa uzalishaji wa maji unavyofanyika kwenye Mtambo wa
maji wa Ruvu Juu wakati wa ziara yake ya kutembelea mitambo ya
uzalishaji maji ya Ruvu Chini na Juu iliyokuwa na lengo la kuona miradi
inayotekelezwa na DAWASA.
Meneja
wa Mtambo wa Ruvu Juu Mhandisi Edward Mkilanya akitoa ufafanuzi kwa
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi(wa pili kulia)
kuhusu mchakato wa uzalishaji wa maji unavyofanyika kwenye Mtambo wa
maji wa Ruvu Juu wakati wa ziara yake ya kutembelea mitambo ya
uzalishaji maji ya Ruvu Chini na Juu iliyokuwa na lengo la kuona miradi
inayotekelezwa na DAWASA.
Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akinywa maji ya
yanayozalishwa kwenye Mtambo wa Maji wa Ruvu ili kutambua ubora wa maji
hayo kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na DAWASA. Wa kwanza
kushoto ni Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Shabani
Mkwanywe.
Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akisaini kitabu cha
wageni alipofika kwenye Mtambo wa Maji wa Ruvu wakati wa ziara yake ya
kutembelea miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA ili kujionea ufanisi
wa Miradi hiyo na kuweza kufikia malengo ya Serikali ya kumtua mama ndoo
kichwani.
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akiendelea na ziara yake kwenye Mtambo wa Ruvu Juu
Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kumaliza Ziara yake kwenye Mtambo wa
Maji wa Ruvu Chini na kujione unavyofanya kazi kwa ajili ya kumtua ndoo
mama mtoni wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali
inayotekelezwa na DAWASA.
Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akitembelea maeneo
mbalimbali ya chanzo cha Maji Ruvu Chini kilichopo wilaya ya Bagamoyo
Mkoani Pwani wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali
inayotekelezwa na DAWASA
Meneja
wa Mtambo wa Ruvu Chini DAWASA Mhandisi Emaculata Paul akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu namna walivyojipanga kutoa huduma ya
usambazaji wa maji kwa kutumia eneo la mto huo kwa ajili ya upatikanaji
wa maji mengi yatakayoweza kutumiwa na wananchi wa Dar es Salaam pamoja
na Bagamoyo wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi
Maryprisca Mahundi (Mb).
Mkurugenzi
wa Uzalishaji na Usambazaji Maji kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa
Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Shabani Mkwanywe akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu DAWASA walivyojipanga kusambaza maji
katika mikoa ya Dar es Salaam pamoja na Pwani wakati wa Ziara ya Naibu
Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi alipotembea mitambo ya Ruvu
Juu na Ruvu Chini
Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kumaliza Ziara yake kwenye Mtambo wa
Ruvu Chini na kufurahishwa na kazi inayofanywa na DAWASA katika
usambazaji wa maji kwa mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Pwani.
Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza jambo na
Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini DAWASA Mhandisi Emaculata Paul
alipotembelea
Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi(kushoto) akizungumza jambo na Meneja Mawasiliano DAWASA, Everlasting Lyaro(kulia) wakazi wa ziara ya kutembelea mitambo ya uzalishaji Maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini ili kuona ufanisi wa miradi hiyo ya maji ya DAWASA.
Ziara ikiendelea
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...