Na Amiri Kilagalila,Njombe
Serikali
mkoani Njombe imezindua mbolea ya asili "Hakika" inayofanya vizuri
kwenye kilimo cha parachichi huku wakulima mkoani humo wakihamasishwa
kutumia mbolea hiyo kutokana na wananchi wengi mkoani Njombe kulima kwa
kiasi kikubwa tunda la Parachchi hivi sasa.
Ili
kuboresha kilimo cha zao la parachichi katika mikoa ya Nyanda za Juu
Kusini, Chuo Kikuu Cha Dar es salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya
Guavay ya Jijini Dar es salaam wamekuja na ubunifu wa kutumia mabaki ya
mimea mbalimbali na kuzalisha mbolea mpya ya Asili inayofahamika kwa
jina la HAKIKA lengo likiwa ni kuongeza tija na ubora wa zao hilo.
Mratibu
wa mradi wa mbolea ya Hakika kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es salaam
Professor Amelia Kivaisi amesema katika utafiti uliofanywa umebaini kuwa
mbolea ya Hakika inasifa ya kuongeza tija ya ukuzaji wa mimea na
kurutubisha udongo ulioharibiwa na kemikali.
"Kwetu
sisi chuo kikuu cha Dar es Salaam hii ni siku muhimu sana na tunatambua
kuwa nchi yetu ya Tanzania ni nchi ya wakulima na wafanyakazi,zaidi ya
asilimia 70 ya watanzania wote wanajishughulisha na kilimo na wanaishi
maeneo ya vijijini"alisema Prof,Amelia Kivaisi
Naye
mratibu wa mradi na mhandisi Ahad Katera ambaye ni mkurugenzi wa
kampuni ya Guavay amesema "Hadi sasa tayari tumekwishawekeza zaidi ya
Bilioni 1.5 katika miundombinu tafiti za masoko malighafi,teknolojia za
kuongeza uzalishaji pamoja na mashamba darasa"
Akiongea
kwa niaba ya wakulima wa Parachichi mkoani Njombe, mmoja wa mashuhuda
wa Matumizi ya Mbolea hiyo Erasto Ngole amekiri kuwa katika Mkoa wa
Njombe iwapo wakulima watapewa elimu kutoka kwa maafisa ugani
watanufaika na matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo zenye kuleta tija
shambani, kauli iliyoungwa mkono na Mbunge wa Njombe Mjini Mheshimiwa
Deo Mwanyika.
"Matokeo
yalikuwa ni ya kuridhisha,na mbolea ilifanya kazi nzuri sana tangu
waliponza kufanyia utafiti shambani kwangu mwaka 2017 na nilipata
matokeo makubwa kwa kuvuna matunda makubwa,mazuri yasiyo na
mabaka"alisema Erasto Ngole Mkulima wa Parachichi
Naye
mbunge wa jimbo la Njombe Mjini Deo Mwanyika alisema "tunataka tupate
bei nzuri ya parachichi zetu na moja ya mambo ambayo kampuni hii ya leo
ambayo imezindua Mbolea na imetuhakikishia kuwa mbolea hii imepata
uthibitisho"
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa mbolea hiyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa
Njombe, Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Bi.Kissa Kasongwa ameipongeza Kampuni
ya Guavay kuja na mbinu mpya ya kuwa na mbolea ya Hakika na kwamba ndani
ya wilaya ya Njombe ambapo mwitikio wa wakulima wa zao la Parachichi ni
mkubwa utaenda kuwanyanyua wakulima.
"Na
nitoe wito kwa maafisa ugani wote kuhakikisha wanawatembelea wananchi
na kuwaeleza vitu muhimu ikiwa ni pamoja na kufuatilia afya ya udongo
"alisema Kissa Gwakisa Kasongwa
Baadhi ya wakulima,viongozi na washiri wa hafla hiyo ya uzinduzi wakiwa
katika zoezi la uzinduzi wa mbolea lillofanyika mjini Njombe na kuwapa
fursa wakulima kunza kuitumia rasmi mbolea hiyo.Bango lenye kuonyesha ubora wa mbolea hiyo shambani kwenye zao la parachichi.
Mbolea ya Hakika iliyokuwa packed kwenye mifuko kwa ajili ya kutumiwa na wakulima.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...