
Meneja wa Masoko na Uhamaishaji wa Self Microfinance Linda Mshana akitoa maelezo kwa mteja aliyetembelea Banda lao ndani ya Jengo la Wizara ya Fedha katika maonesho ya Biashara ya 45 ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
MFUKO wa Self Microfinance Fund umelenga kuongeza wigo na kuwapa fursa ya kukuza mtaji kwa wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa ili kuongeza ajira kwa watanzania hususani vijana.
Katika maonesho ya biashara ya 45 ya kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam, mfuko huo umelenga zaidi katika kutoa mikopo kw wananchi,taasisi za kiserikali, asasi za kifedha, Kilimo na biashara.
Akizungumza na Michuzi Blog, Afisa Masoko na Mhamasishaji wa Self Microfinance Linda Mshana amesema katikai wao wanatoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo,wa kati na wakKubwa ili waweze kujikuza kiuchumi katika biashara zao.
Mshana amesema, mikopo hiyo inawawezesha wafanyabishara kukuza mitaji yao sambamba na wakulima kulima kilimo cha kisasa na uhakika.
Amesema, mikopo yao inapatikana kwa masharti nafuu na wanawakaribisha asasi za kifedha kama vikundi vya SACCOS kuja kupata mikopo ili wakuze mitaji yao na wengine kuanza biashara.
Mshana amewataka watanzania kujitokeza katika banda lao lililopo ndani ya Jengo la Wizara ya Fedha ili kupata maelezo mbalimbali na kufahamu zaidi kuhusu Self Microfinance na huduma za kifedha wanazozitoa.
Kwa upande wa Mnufaika, George Buchafwe amesema Self Microfinance Fund imewanufaisha wajasiriamali wadogo na wa kati kwa kuwapatia mikopo iliyowawezesha kununua vitendea kazi vitakavyomuwezesha mjasiriamali kujiendeleza kiuchumi.
Buchafwe amesema, kwa kuwawezesha wajasiriamali wameweza kununua mashine mbalimbali kama za kukamulia mafuta ya alizeti, kusaga na nyinginezo.
Amesema, uwezeshaji huo umeongeza soko la ajira, na hata kuongeza pato la Taifa ikwa bidhaa mbalimbali kutengenezwa ndani ya nje na kuacha kuingiza vitu kutoka nje.
Kwa sasa Self Microfinance inapatikana katika ofisi zake zilizopo Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya na Kahama na pia wanapatakina kwenye mitandao ya kijamii kwa jina la Self Mf.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...