BAADA ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo ameongoza viongozi mbalimbali wa serikali na kidini, wasanii na wanahabari kupata chanjo ya UVIKO-19 katika Ikulu ya Dar es Salaam ikiwa ni uzinduzi rasmi wa kuendelea kufanyika kwa zoezi hilo nchini, Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimempongeza kwa hatua hiyo muhimu.

Wengine waliochanjwa ni waziri mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, katibu mkuu kiongozi, viongozi wa kisiasa akiwemo katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka, viongozi wa dini, waziri wa afya Dkt Doroth Gwajima, makatibu wakuu wa wizara,  waandishi wa habari, baadhi ya wasanii na viongozi wengine mbalimbali waliokuwepo.

Wakati anazindua chanjo hiyo , Rais Samia amewahakikishia watanzania chanjo ni salama na lengo la kila chanjo ni kuwakinga watu dhidi ya maambukizi na hivyo basi kuokoa maisha kwa mantiki hiyo amewaomba wachanjwe dhidi ya virusi hivyo japo ni hiari kufanya hivyo.

"Mimi ni Mama wa Watoto 4, Bibi wa wajukuu, mke lakini pia Rais na Amir Jeshi Mkuu nisingejitoa mwenyewe kujipeleka kwenye kifo nikijua nina majukumu yote haya, hii chanjo ni salama  na wataalamu wetu wamejiridhisha, NIKO TAYARI Kuchanjwa, naomba mniunge mkono" Rais Samia

Akizungumza baada ya kuchoma chanjo hiyo mara baada ya  uzinduzi uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka alisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hatua hii muhimu ndani ya Taifa la Tanzania.

"CCM inampongeza Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ibara za 83(o) na 84." alisema Shaka

Alisisitiza tuliahidi CCM itaimarisha huduma za afya kwa watanzania sambamba na kuimarisha mifumo na miundombinu ya kuwakinga dhidi magonjwa ya mlipuko ikiwemo UVIKO-19.

"Alilofanya Rais Samia leo ni utayari wake na nia yake thabiti katika kuwatumikia watanzania na kuliongoza Taifa likiwa salama zaidi ameonesha uaminifu wake katika kutimiza ahadi. Uongozi ni kuonesha njia ndivyo alivyofanya Rais Samia na ndio maana viongozi na wasaidizi wake tumemuunga mkono kupata chanjo hii ya UVIKO 19 hapa ikulu. Tuwaombe wananchi waendelee kupata taarifa sahihi na wafanye uamuzi sahihi wa kupata chanjo hii. Kinga ni bora kuliko Tiba." Alisema Shaka

Serikali ameponfeza utaratbu wa serikali wa kutoa kipaumbele watu walio katika hatari ya maambukizi wakiwemo wazee na wote walio mstari wa mbele katika kuwahudumia wananchi katika awamu hii ya kwanza ya dozi takribani milioni moja zilizowasili.


 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Shaka Hamdu Shaka akichoma chanjo ya Corona leo Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua utoaji chanjo hiyo kitaifa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...