Na Khadija Seif, Michuzi TV

WJASIRIAMALI kutoka Unguja visiwani Zanzibar wametumia kongamano la kwanza la Taasisi ya The Warrior Women kubainisha changamoto zao katika kupata Masoko na mitaji ya kukuza Biashara zao.

Akizungumza na Michuzi TV leo Julai 28,2021, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Sabra Machano mara baada ya kufanyika kwa kongamano hilo wajasiriamali mbalimbali wameweza kuzungumza vitu mbalimbali  ikiwemo upatikanaji wa fursa za biashara hususani masoko na mitaji.

Amesema kuwa taasisi hiyo imejikita katika kutatua changamoto za wajasiriamali,kuwapatia Ushauri ,elimu pamoja na kutatua ufumbuzi wa baadhi ya changamoto ambazo zinahitajika nguvu zaidi kutoka katika Mamlaka husika na amewaahidi wajasiriamali kupata elimu ya kibiashara pamoja na kuwasaidia kupata mitaji ya kibiashara .

 "Kongamano limepata muitikio mzuri na imeonyesha kwa kiasi gani wajasiriamali wamekua wakihitaji kupatiwa fursa au platform ambayo itawaweka pamoja na kujifunza vingi huku swala la kupanua Masoko na mitaji ikipewa kipaumbele hasa visiwani Zanzibar".

Aidha, Mkurugenzi huyo ameeleza Sababu ya kuwepo watu maarufu kama Muimbaji wa taarab Isha Mashauzi, Mbunifu Martini Kadinda na wengine wengi kwenye kongamano Hilo.

 "Kupitia kongamano letu linalokwenda kwa kauli mbiu ya "Chonga barabara" tuliona ni vizuri kuwepo viongozi na watu maarufu ili waweze kuwapa Moyo wajasiriamali ili kuona jinsi walivoanza safari zao Hadi walipofika pamoja na kuwaonyesha jinsi ya kutafuta Masoko ya kibiashara zaidi."

 Hata hivyo ameongezea kuwa Taasisi hiyo kwa Sasa Ina wajasiriamali mbalimbali ikiwemo Nass product ambae anatengeneza juisi za matunda na mbogamboga pamoja na Manju duox anaetengeneza viungo vya chakula.

 Na kwa Sasa kongamano hilo limefanyika Unguja na katika kipindi kijacho litafanyika Pemba na kuwaasa wajasiriamali kuzikimbilia fursa za kibiashara na kujitanua kimasoko.

Mkurugenzi wa Taasisi ya The warrior Women Sabra Machano akizungumza na wajasiriamali mbalimbali waliojitokeza katika kongamano la kwanza lililopewa kauli mbiu ya "Chonga barabara" lililofanyika katika chuo Cha utalii Maruhubi unguja visiwa vya Zanzibar
 Wageni waalikwa waliohudhuria kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya The warrior Women lililofanyika katika chuo Cha utalii Maruhubi unguja visiwa vya Zanzibar ambao kongamano la pili linatarajiwa kufanyika pemba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...