Charles James, Michuzi TV

HAWANA Bahati! Ndivyo unavyoweza kusema kuwa Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wamekua hawana bahati ya kupata ushindi kwenye michezo yao ya hivi karibuni ambayo imehudhuriwa na viongozi wa juu wa Nchi yaani Rais.

Katika michezo mitatu ya mwisho ambayo viongozi hao kwa nyakati tofauti wamejitokeza kwenye michezo ya Simba mabingwa hao mara tatu mfulululizo wa Ligi Kuu Tanzania wameipoteza kila mmoja kwa goli 1-0.

Mchezo wa kwanza kwa Simba kupoteza mbele ya kiongozi mkuu wa nchi ulikua dhidi ya Kagera Sugar Mei 20, 2018 ambapo walifungwa bao 1-0 mbele ya aliyekua Rais Hayati Dk John Magufuli kiasi cha Rais kusema kuwa Simba imetobolewa tundu huku akiishauri kufanyia mabadiliko kikosi chao ili iweze kufanya vizuri kimataifa.

Katika mchezo huo Simba tayari ilikua imeshatwaa ubingwa wa Ligi lakini Kagera wakaharibu rekodi yao ya kumaliza msimu bila kufungwa.

Mchezo mwingine Simba waliupoteza dhidi ya mahasimu wao wakuu, Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu mbele ya Hayati Rais Magufuli kwa bao 1-0 goli lililofungwa kwa njia ya faulo na Benard Morrison ambaye kwa sasa anaichezea Simba.

Katika mchezo huo Hayati Dk Magufuli aliingia uwanjani akiwa amevaliwa jezi yanye upande mmoja rangi ya Simba na mwingine ukiwa na rangi ya Yanga.

Muendelezo wa Simba kutopata ushindi mbele ya Marais umeendelea tena leo baada ya kufungwa na mahasimu wao, Yanga kwa bao 1-0 mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alifika uwanjani hapo kwa 'surprise'.

Goli la Yanga kwenye mchezo wa leo limefungwa na kiungo wake Zawadi Mauya katika dakika ya 12 ya mchezo huo wa Ligi.

Matokeo hayo yanaifanya Simba iendelee kusubiri kutangaza ubingwa wake kwani kama ingeshinda leo ingefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya nne mfulululizo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...