Florence Masuka (wa kwanza kulia)  Mwenyekiti Jumuiya ya wazazi Mkoa wa Dar es Salaam akipata maelezo katika Banda la STAMICO kwenye Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.


Na Said Mwishehe, Michuzi TV

VIONGOZI wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania(UWT) kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam wametembelea mabanda mbalimbali yaliyoko katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Mwalim Nyerere.

Miongoni mwa mabanda yaliyotembelewa na viongozi hao wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam akiwemo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Tifa ya  CCM(NEC) Angel Akilimali ni banda la Shirika la Madini la Taifa(STAMICO).

Wakiwa hapo maofisa na watalaam wa STAMICO wa kada mbalimbali walitumia nafasi hiyo kuwaeleza viongozi hao wa UWT shughuli wanazozifanya huku wakionesha wakiwaonesha sampuli za makaa ya mawe ambayo yanatumika kutengeneza mkaa mbadala ambayo yalionekana kuwavutia viongozi hao na kutaka kujua faida zake na jinsi yanavyotumika.

Akifafanua zaidi, sababu za kuamua kutembelea banda hilo la STAMICO, Akilimali amesema pamoja na mambo mengine shirika hilo limekuwa likiendeleza wachimbaji wadogo wa madini na kuwajengea uwezo wa kuchimba madini katika mazingira yasiyo hatarishi kiafya.

"Tunawashuku STAMICO kwa kupata fursa ya kutembelea hapa pamoja na mabanda mengine yaliyomo humu, tumekutana na wajasiriamali wanawake , tumejifunza na kupata uzoefu wao katika shughuli wanazofanya zikiwemo katika sekta ya madini.

"Lakini kwenye sekta ya madini akina mama wengi walikuwa bado waoga wanaogopa, walikuwa hawana muamko, hivyo kwa kutembelea kwetu tukitoka hapa tunakwenda kuhamasisha wanawake wa UWT ili waweze kukimbilia fursa hiyo.

"Wanawake wasiogope kwani wanaweza, na kama katika mabanda hayo ya madini kuna wanawake ambao wameweza basi na wanawake wengine wanaweza, hivyo ni kuchangamkia fursa kwa kujitokeza kufanya shughuli za uchimbaji madini,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...