Mwalimu wa VETA Chang'ombe,Ally Issa akionesha umahiri wa Dawa za kuua wadudu chooni katika maonesho Sabasaba ndani ya Banda la VETA.
Mwalimu wa VETA Chang'ombe Ally Issa akizungumza  na wanafunzi kuhusiana na Dawa ya kuua wadudu chooni  waliotembelea Banda la VETA  maonesho ya Sabasaba

*Hiyo kuwa dawa ya kwanza kuzalishwa Tanzania kwa kuua wadudu chooni.

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MAMLAKA ya Elimu n a Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA kupitia Chuo cha VETA Chang'ombe wamegua Dawa ya kupulizia chooni kwa ajili ya kuua bakteria wanaosababisha ugongwa wa maambukizi ya njia ya mkojo (UTI).

Akizungumza katika maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) Mwalimu wa Chuo hicho, Ally Issa amesema kuwa waliamua kufanya utafiti na kubaini hakuna dawa ya kuua wadudu wanaosabisha UTI Tanzania nzima.

Amesema dawa hiyo ina manukato na kusafisha matundu ya choo ya sinki vile vile inaua bakteria.

Issa amesema kuwa dawa hiyo iko katika uangalizi na Mmalaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) katika hatua mwisho wakiwa wamepata cheti cha uchunguzi na kibali cha muda cha Maonesho ikiwa tayari itaingia sokoni.

Amesema kuwa kumekuwa na changamoto nyingi ya ugonjwa UTI na kuamua kutatua changamoto katika jamii dhidi ya ugonjwa huo.

Aidha amesema kuwa VETA inaangalia nguvu kazi ambapo watu wakiwa na changamoto za kiafya hawawezi kuzalisha na hatimae Taifa haliwezi kupata mapato kutokana na nguvu kazi hiyo.

VETA Chang'ombe licha ya kufundisha katika Mafunzo mbalimbali wanaangalia changamoto zinazowakabili jamii na kutafuta suluhisho.

Amesema kutokana na Kauli mbiu ya maonesho 45 ni Uchumi wa Viwanda kwa ajira na biashara endelevu inasaidia vijana kupata ajira kwa kupata Mafunzo ya utengenezaji wa dawa hiyo na kuingiza sokoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...