Watanzania wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona (COVID-19,) kwa kuzingatia taratibu zinazotolewa na Wizara ya Afya pamoja na elimu ambazo zimekuwa zikitolewa kwa ushirikiano na wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini.
Akizungumza na kituo cha ITV jijini Dar es Salaam Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema kuwa jamii lazima ielewe kuwa hali imedhibitiwa, ila kasi ya wagonjwa inazidi kujitokeza kwa wagonjwa kulazwa katika hospitali mbalimbali.
Dkt.Gwajima amesema watu wasidhani kuwa kazi itafanyika maiti zikianza kuzagaa barabarani, bali jitihada zinazofanywa na Serikali na Wizara ya Afya ni kuhakikisha jamii haipati athari na wimbi la tatu na virusi vya Corona.
"Wagonjwa wapo wanaendelea kujitokeza, maambukizi yapo, nguvu kubwa inafanyika na wataalamu wa afya ili kuzuia hali mbaya isitokee." Amesema.
Pia amewataka wananchi wasioitikia tahadhari zinazotolewa na wataalamu wa afya kuitikia tahadhari hizo ili kuweza kuepuka na kuwaepusha wengine dhidi ya maradhi hayo.
Vilevile Dkt.Gwajima amesema miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya ikifuatwa wimbi la tatu la maambukizi ya Corona halitaleta athari na hiyo ni pamoja na kila mmoja kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni, kutumia vitakasa mikono (sanitizer,) kuzingatia mlo kamili pamoja na kufanya mazoezi

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...