Na Humphrey Shao,Michuzi TV Dar es Salaam

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya  Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto .Prof. Abel Makubi, amezindua zoezi la  usambazaji wa chanjo  ya UVIKO 19 aina ya Jonson Jonson  Kwenye BOHARI ya Dawa (MSD) iliyopo Keko Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada uzinduzi huo Prof .Makubi  amesema chanjo hizo zitasambazwa  katika mikoa yote 26     ya Tanzania Bara.

"Chanjo hizi ni Bure na zitapatikana katika Hospitali zote zitakazo elekezwa  za Serikali na zile za Binafsi ambazo zitakuwa zimeteuliwa" Amesema Prof Makubi.

Amesisitiza kuwa chanjo hiyo ni Bure na Serikali imesambaza katika mikoa yote kwa idadi tofauti kulingana na visa vilivyoripotiwa katika mkoa huo.

Ametaja kuwa chanjo hii inaanza kutolewa kwa makundi maalum ambayo ni  Wazee ,Watumishi , Watumishi wa majeshi  na Wenye magonjwa hatarishi.

Kwa upande wake Kaimu  Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Dr.Benjamini Hubila amesema mchakato wa usambazaji umekamilika na shirika lake limejipanga vyema kupeleka chanjo hizo kwa wakati.

Amesema MSD itasambaza chanjo hizo ndani ya siku Saba kwa kupitia mtandao wake wa usambazaji dawa nchini

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Prof.Abel Makubi  akionesha  chanjo aina ya Jonson Jonson kwa Wana habari.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Prof.Abel Makubi  akikabidhi  chanjo kwa  Mkurugenzi wa MSD Dr.Benjamini Hubila.

Wafanyakazi wa MSD wakifungua majokofu yanayotumika kuhufadhia chanjo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Prof.Abel Makubi  akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa usambazaji wa chanjo ya uviko 19 .
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD nchini, Dr.Benjamini Hubila akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa habari.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...