Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Beng'i Issa(kushoto) na Mkurugenzi wa Purple Planet Hilda Kisoka(kulia) wakiwa wameshika Jarida Maalum la Wanawake 2021 ambalo limezinduwaliwa jijini Dar es Salaam.Katikati ni Shamim Khan ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu katika Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA)aliyekuwa ni miongoni mwa walialikwa kushuhudia uzinduzi wa jarida hilo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Beng'i Issa(kushoto) akijiandaa kukata utepe kama ishara ya uzinduzi wa jarida la Maalum la Wanawake 2021 .Kulia ni Shamim Khan ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu katika Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA).
Beng'i Issa ambaye ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC), akiwa na Mkurugenzi wa Purple Planet Hilda Kisoka(wa pili kulia) pamoja na Shamim Khan ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu katika Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakisikika kwa katika jarida hilo ambalo pia lipo katika mfumo wa mtandao.
Sehemu wageni waalikwa waliokuwa kwenye tukio hilo la uzinduzi wa jarida la wanawake 2021 wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa uzinduzi huo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Beng'i Issa(kulia) , Mkurugenzi wa Purple Planet Hilda Kisoka(katikati) na Lazaro wakipiga makofu kuashiria kushangalia jambo wakati wa uzinduzi huo .
Beng'i Issa ambaye ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC)akifafanua jambo kabla ya kuzindua rasmi jarida la wanawake 2021 .Katikati ni Mkurugenzi wa Purple Planet Hilda Kisoka(katikati).
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu katika Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA) Shamim Khan akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Beng'i Issa(kulia)akimkabidhi jarida maalum la wanawake 2021 mwanasiasa mkongwe ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali serikali Shamsa Mwangunga.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Beng'i Issa(wa kulia waliokaa)akiwa pamoja na viongozi wengine kwenye meza kuu wakiwa na baadhi ya watumishi wa Pirple Planet waliosimama nyuma wakionesha jumbe mbalimbali wakati wa uzinduzi wa jarida hilo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Beng'i Issa(wa pili kulia), akiwa na viongozi wengine wakati wa uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu katika Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA) Shamim Khan(kulia) akikabidhiwa jarida maalum la wanawake 2021 na Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Beng'i Issa(kushoto)
Katikati ni Mkurugenzi wa Purple Planet Hilda Kisoka(kushoto) akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi huo.Katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Beng'i Issa na kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu katika Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA) Shamim Khan.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Beng'i Issa akitoa tuzo kwa mmoja ya wanawake ambao mchango wao umetaliwa na Purple Planet katika harakati za kumkomboa wanawake nchini.
Msichana Getrude Mligo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Have all creative agency akipokea tuzo kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Beng'i Issa.Tuzo hiyo ni ya kutambua mchango wa wanawake na wasichana katika kuleta maendeleo ya wanawake nchini.
Baadhi ya waliotunukiwa tuzo kutokana na mchango wao katika maendeleo ya wanawake nchini wakiwa wamesimama nyuma ya meza kuu wakiwa wameshika tuzo hizo ambazo wamekabidhiwa wakati wa tukio la uzinduzi wa jarida maalum la wanawake 2021.


Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) Beng'i Issa amezindua Jarida Maalum la Wanawake 2021 ambalo linatarajia kusomwa na watu zaidi ya 100,000 kupitia nakala ngumu,na kidigitali  huku akitumia nafasi hiyo kuelezea hatua mbalimbali ambazo zimeendelea kufanywa na Serikali katika kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Jarida hilo ambalo limesheheni fursa na taarifa mbalimbali kwa wanawake na wasichana limezinduliwa limezinduliwa jijini Dar es Salaam na limeandaliwa na THE PURPLE PLANET chini ya Mkurugenzi wake Hilda Kisoka.

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa jarida hilo maalum la wanawake,Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Being Issa amesema  amekuwa akifurahishwa na kazi ambazo zinafanywa na Purple Planet tangu wameanza na wamekuwa wakishirikiana kwa karibu, hivyo amewapongeza kwa jitihada zao zenye viwango vya hali ya juu."Hilda ni msichana anapenda kujifunza sana na anatumia uwezo wake mzuri ambao Mungu amemjalia, ana mahusiano mazuri na watu, amefanya kazi na wanawake wengi na wamefanikiwa."

Aidha amesema  mwanamke ni mtu muhimu kama jamii inavyofahamu , kwa hata wanaume hapo walipo wamezaliwa na  na mwanamke, wamelelewa na mwanamke na ndio maana Serikali imeamua kuwekeza nguvu zake katika kusaidia mwanamke kiuchumi ,kwa kutambua akisaidiwa mwanamke kiuchumi unakuwa umeondoa matatizo mengi."Kwa hiyo kama Rais alivyosema Tanzania inataka kuwa Champion katika suala la haki za wanawake na sisi ndio tunaomsaidia Rais tutahakikisha hili linafanyika."

Amefafanua kuna mambo mengi yanayozungumzwa mwanamke yakiwemo ya mazingira yanayosababisha kumkwamisha kutokana na mila na desturi za kiafrika ambazo wakati mwingine  zinamfanya mwanamke kushinda kumiliki ardhi na mambo mengine katika jamii.Hivyo wanawake wengi wameshindwa kumiliki rasilimali na matokeo yake wanabaki nyuma na kushindwa kusonga mbele lakini Serikali imekuwa ikiangalia kwa karibu mambo hayo ili nao wafunguliwe milango ya kiuchumi.

Kuhusu jarida ambalo amelizindua amesema linakwenda kufungua fursa kwa wanawake kokote aliko kwani jarida hilo litatangaza bidhaa za watu mbalimbali , na litafahamisha umma wa watanzania vitu gani vinaweza kupatikana na vinatipatikana wapi."Hili ni jambo nzuri sana na hata vitabu vya dini vinasema mafanikio yako ndani ya kwenye kusoma, hivyo jarida hili linakwenda kutengeneza utaratibu mzuri wa watu kupenda kusoma maarifa".

Ameongeza kupitia jarida hilo watu watajifunza kupitia wengine ambao wamefanya vizuri kiuchumi, kijamii na kimaendeleo na katika maisha lazima awepo mtu ambaye ataangaliwa kama mfano wa kuigwa huku akisisitiza binadamu wamekuwa na tabia ya kukata tamaa lakini kupitia jarida hilo watakutana na wananawake ambao hawajakata tamaa na leo wamefanikiwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Purple Planet Hilda Kisoka amesema pamoja na juhudi zinazofanywa na Serikali suala la mitaji na dhamana bado ni changamoto, licha ya juhudi na ushiriki wa mwanamke katika shuhuli za kiuchumi bado wanaomiliki ardhi ni asilimia nane na wanaomiliki nyumba na mali zingine zinazoweza kutumika kama dhamana ni asilimia saba tu.

"Tunaomba wakati kamati inaendelea na kazi hii tunayoamini itazaa matunda Ofisi yako yako kwa kushirikiana na wizara zingine ione namna wanawake wanaweza kupata mitaji yenye masharti nafuu kwani ile asilimia nne kutoka katika halmashauri inaweza kusaidia ila kwa wale wafanyabiashara wakubwa na wenye tenda bado ni changamoto hasa wakati huu ambao biashara nyingi zimeporomoka kutokana na janga la corona na wanawake katika ajira na biashara nao ni wahanga wakubwa .

"Kwa kutambua kuwa katika kufikia lengo la ukuaji wa Uchumi kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2025, sekta binafsi inatoa mchango mkubwa, na uwekezaji biashara ni kiungo muhimu, wanawake waliopo katika sekta binafsi wana mchango wa moja kwa moja, hivyo ni muhimu kuendelezwa na kujengewa uwezo katika nyanja mbalimbali nasi pamoja na makongamano semina.

"Pia mafunzo na ushauri na mbinu nyingine za uwezeshaji tumeona kutumia njia ya kuandika makala mbalimbali ,kutambua na kutambulisha wanawake na wasichana mbalimbali wanaofanya vizuri tunaweza kuongeza tija katika kutimiza maelengo endelevu hasa lengo namba 4 la kupata elimu na mafunzo, lengo namba 5 la kupata usawa na malengo mengine yanaendana na hayo. 

"Na kwa umuhimu huu unafanya tukutane hapa leo kuzindua Jarida maalum la wanawake 2021 ambalo tunalotarajia litasomwa na watu zaidi ya 100,000 kupitia nakala ngumu, na kidigitali na kupitia vyombo vya habari tunaupasha uma kuwa jarida hili halitauzwa.Jarida hili limesheheni fursa na taarifa mbalimbali,"amesema Kisoka.

Ameongeza kwenye jarida hilo kuna makala maalum zilizoandikwa na wataalam, kama Uuchumi na biashara,teknolojia, mwanamke na uongozi, maendeleo ya mwanamke katika ajira na maendeleo ya mtoto wa kike."Katika jarida hili tumetambua wanawake na wasichana 10 wenye ushawishi wa maendeleo kwenye sekta mbalimbali, na hatukuacha nyuma wanaume wanaounga mkono juhudi za mwanamke namtoto wa kike.

"Utambuzi wa wanawake na wasichana hawa ulifanyika baada ya kupokea maoni na mapendekezo kutoka kwa wadau ambapo walipendekezwa wanawake na wasichana zaidi ya 400 kupitia mitandao na ujumbe za simu ,emeli na mapendekezo ya moja kwa moja na baadae kamati ilikaa kwa kuzingatia vigezo na kupata wanawake 10, wasichana 10 na wanaume 5 kuwakilisha wengine wengi wanaofanya vizuri hapa nchini na lengo ni kuwapa motisha na kuwaonyesha kuwa jamii inatambua kazi nzuri wanazofanya na tutaendela kufanya hivi kadiri tutatakavyojaliwa,"amesema.

Amesisitiza kufanikisha kwa jarida hili kunaweka msingi wa majarida mengine yatakayobeba dhimambalimbali lengo ni kuhamasisha na kuelimisha jamii pamoja na kufiksha taarifa na fursa  mbalimbali. Kuhusu Purpleplanet Kisoka amesema walianza shughuli zao mwaka 2017 na kutoka hapo wamekuwa wakitoa mafunzo na ushauri kwa wanawake na wasichana na mpaka sasa wamewafikia mojamoja wanawake zaidi ya 5,000 na wanawake zaidi ya 100,000 kupitia mtandao katika mikoa 16 na wengine kutoka nje ya nchi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...