Katibu Mkuu wa CCM akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndg Masanja Kadogosa mara baada ya kuhitimisha Ziara ya Kukagua Mradi wa SGR alioanzia Mkoani Morogoro hadi jiji la  Dar Es Salaam katika Stesheni ya Mpya ya SGR Tazara.

Katibu Mkuu wa CCM akisikikiza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndg Masanja Kadogosa wakiwa safarini kitokea Mkoani Morogoro kuelekea Dar Es Salaam katika treni ya Uhandisi

................................................................................................................
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza viongozi wa chama hasa kupitia Kamati za Siasa katika ngazi za wilaya na mikoa ndani ya siku 14 wakamilishe kukagua miradi yote ya maendeleo ambayo ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 katika maeneo yao na taarifa ya kilichojiri iwasilishwe ofisini kwake.

Sambamba na maagizo ya kuwataka kukagua miradi ya maendeleo, Chongolo pia amewaagiza kuwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa ilani na amesisitiza kuwa chama kitafuatilia utekelezaji wa maagizo hayo. 

Chongolo ametoa maagizo hayo leo tarehe 10 Agosti, 2021 mkoani Morogoro wakati akikagua mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa  (SGR), akiwa ameambatana na Wajumbe wa Sekreterieti ya Chama Taifa.

"Niwapongeze watu wa Morogoro kwani mmeweza kuonesha njia nami nimeamka nije hapa na sekretarieti yangu kujionea kama kinachofanyika hapa ni kile kilichoelekezwa katika ilani yetu ya uchaguzi na ndicho kinachoelezwa kila mara,"amesema Chongolo na kuongeza "Haya ni maagizo na maelekezo Kama tulivyopeana mara baada ya mkutano mkuu maalum kuwa wote tushuke chini kukagua miradi ya maendeleo katika maeneo yetu ."

Amesema wao wanawajibu wa  kuisimamia Serikali na utekelezaji wa Ilani kwani ni sisi ndio tutakaorudi kuwaeleza wananchi nini tumefanya.

Kwa upande wake Mkurungezi Mkuu wa Shirika la Reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa amesema anaishikuru Serikali kwa kuwapatia fedha kwa wakati kwa ajili ya kukamilisha mradi huo huku akifafanua mpaka sasa wamelipa  hati 34 kati ya 35 huku hiyo moja ambayo inalipwa muda wowote kuanzia sasa.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo pamoja na wajumbe wa Sekretariet ya CCM na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Morogoro wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli last Taifa Ndg Masanja Kadogosa wakati wakikagua handaki namba 2 lililopo kijiji cha Mzaganza lenye ukubwa  wa kilomita 1.031.



Wajumbe wa Sekretariet wakiwa katika treni ya Uhandisi kutoka morogoro kihonda hadi dar es Salaam kwanza kulia ni katibu mkuu wa UWT Taifa dkt Philis Nyimbi ,Kenani kihongosi katibu Mkuu wa UVCCM Pamoja na Katibu wa Sekretarieti ya CCM ndg Salum Reja.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo pamoja na wajumbe wa Sekretariet ya CCM na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Morogoro wakitazama Treni ya Wahandisi kabla ya kuanza Safari kwa kutumia Usafiri huo kutokea Mkoani Morogoro kwenda Mkoa wa Dar Es Salaam.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo (Kushoto) akifurahia Jambo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe, Martin Shigela  Pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo pamoja na wajumbe wa Sekretariet ya CCM na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Morogoro wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli last Taifa Ndg Masanja Kadogosa wakati wakikagua Stesheni ya SGR Kihonda Mkoani Morogoro.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo pamoja na wajumbe wa Sekretariet ya CCM na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Morogoro wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli last Taifa Ndg Masanja Kadogosa wakati wakikaguawakikagua Stesheni ya SGR Kihonda Mkoani Morogoro..

Picha ya Pamoja ya Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM wakiwa nje ya Handaki namba 2 lililopo kijiji cha Mzaganza lenye ukubwa  wa kilomita 1.031.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo pamoja na wajumbe wa Sekretariet ya CCM na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Morogoro wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli last Taifa Ndg Masanja Kadogosa wakati wakikagua handaki namba 2 lililopo kijiji cha Mzaganza lenye ukubwa  wa kilomita 1.031.


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo pamoja na wajumbe wa Sekretariet ya CCM na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Morogoro wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli last Taifa Ndg Masanja Kadogosa wakati wakikagua handaki namba 2 lililopo kijiji cha Mzaganza lenye ukubwa  wa kilomita 1.031.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Daniel Chongolo pamoja na wajumbe wa Sekretariet ya CCM na Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Morogoro wakisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli last Taifa Ndg Masanja Kadogosa wakati wakikagua handaki namba 2 lililopo kijiji cha Mzaganza lenye ukubwa  wa kilomita 1.031. (PICHA ZOTE NA CCM MAKAO MAKUU).
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo akiambatana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmshauri Kuu ya CCM ya Taifa ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ambapo, akizungumza katika kikao cha mapokezi ametoa siku 14 kwa kamati za Siasa nchi nzima kuwasilisha taarifa za ziara za ukaguzi wa miradi na shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Ametoa maagizo hayo katika kikao cha mapokezi na viongozi wa Chama na Serikali mkoani Morogoro na watendaji wa Shirika la Reli, wakati wakitembelea mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kuanzia Kilosa Morogoro mpaka kituo cha Reli ya Kisasa mkoani Dar es salaam leo tarehe 10 Agosti, 2021.

"Tumefanya uamuzi wa kuja wote ili kuweka msisitizo, suala la ukaguzi wa miradi ya maendeleo ambayo ipo na ilitolewa ahadi kwenye Ilani yetu ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025 ikiwemo mradi huu wa reli ya kisasa. Tumekuja kuhakikish miradi hii inakaguliwa na kamati zetu za siasa kote nchini."

Aidha Katibu Mkuu katika maelekezo hayo, ameeleza kuwa, "Napata taarifa kuna baadhi ya mikoa na wilaya bado wanavutana lini waende kutembekea miradi, sasa naagiza, na ni wajibu wa ngazi zote kutekeleza, wale ambao bado ninawapa siku 14 wawe wametekeleza na walete taarifa hizo za miradi na twende katika hatua nyingine, hatuwezi kuwa tunasubiri kila siku kutekeleza jambo moja."

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi huo wa Reli ya Kisasa.

"Wakati mnatuwasilishia taarifa nilikuwa naangalia mambo matatu, la kwanza, nilitaka kujiridhisha je fedha zinakuja? Mmenihakikishia kuwa, fedha zote ambazo mlikuwa mnahitaji ili kuendelea na ujenzi na kuanza ujenzi kule Kisaka tayati malipo yameanza kutolewa kwa kasi kubwa, hongereni sana na niwapongeze sana serikali kwa hilo na nimpongeze sana Mhe. Rais wetu kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli hii ya Kisasa."

Ukaguzi wa mradi huo, umeanzia eneo la Kilosa mkoani Morogoro na kuendelea katika maeneo ya Pugu na kuhitimishwa katika kituo cha Reli ya kisasa Mkoani Dar es salaam.

Ziara hii imejumuisha wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa akiwemo Naibu Katibu Mkuu (Bara) Ndg. Christina Mndeme, Makatibu wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, Oganaizesheni Ndg. Mauldine Castico,  Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Lubinga na Makatibu Wakuu wa Jumaiya za CCM, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndg. Kennan Kihongosi, Katibu Mkuu wa Wanawake Dkt. Philis Nyimbi na Katibu Mkuu wa Wazazi Ndg. Gilbert Kalima.
 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...