Na Amiri Kilagalila,Njombe.
Waziri
wa Nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa Mhe. Ummy
Mwalimu,ameahidi kutoa vifaa tiba vyenye thamani ya Milioni 300 kwa
ajili ya kituo cha afya Makowo halmashauri ya mji wa Njombe kilicho
kamilika kwa asilimia 100 tayari kwa ajili ya kuweza kutoa huduma ya
matibabu.
Ummy ametoa
ahadi hiyo alipofika katika halmashauri hiyo na kuzungumza na watumishi
pamoja na kuweka jiwe la msingi katika kituo hicho cha afya kilichopo
katika kata ya Makowo.
"Naahidi
vifaa tiba vya shilingi milioni 300 kuwaunga mkono wana Makowo na jambo
la pili la watumishi kwa bahati nzuri tutapata ajira mpya kwa hiyo
tutahakikisha tunaweka orodha kuwa tuna kituo cha afya Makowo kinahitaji
watumishi kwa hiyo na watumishi wa afya tunawaletea"alisema Ummy
Mwalimu
Aidha waziri Ummy
ameahidi gari ya kubeba wagonjwa katika kituo hicho kutokana na ombi
kubwa la wakazi wa kata hiyo wanaosafiri umbali mrefu kufuata huduma za
afya.
"Tunaahidi gari ya
wagonjwa Land Cruser na mama Samia amesema Kazi iendelee kwa hiyo
tunawaletea gari ya wagonjwa lakini swala la umeme nimelipokea naenda
kuwa barozi wenu kwa waziri wa nishati"aliongeza Ummy
Awali
mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya kwa niaba ya wananchi wa
kata hiyo alisema alikuwa akisumbuliwa na viongozi wa halmashauri hiyo
juu ya Mambo hayo matatu ya muhimu katika kituo cha afya ili kiweze
kuanza kutoa huduma kea wananchi.
"Watu
wanne akiwemo diwani wa hapa, mkurugenzi pamoja Mbunge wamekuwa
wakinisumbua sana kwa ajili ya vifaa tiba,gari la kubeba wagonjwa,umeme
na watoa huduma za afya.Nina uhakika wananchi wa Makowo wanakwenda
kupona"alisema Rubirya mkuu wa mkoa wa Njombe
Naye
mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe Jassel Mwamwala licha
ya kupongeza juhudi za wananchi katika ujenzi wa kituo hicho cha afya na
kuahidiwa kuletewa vifaa tiba ili kiweze kuanza kutoa huduma,ametoa
wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
Kituo
cha afya Makowo kilichokamilika mkoani humo kinatajwa kujengwa kwa
ghalama ya milioni 598 huku zaidi ya milioni 40 zikiwa zimetokana na
nguvu ya wananchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...