Na Karama Kenyunko,Michuzi TV

MASHAHIDI 24 wa upande wa Mashitaka akiwemo Kamishna wa Polisi Robert Boaz  na Luteni Denis Urio wanatarajia kutoa ushahidi katika kesi ya tuhuma za uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi  inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA)Freeman Mbowe  wenzake watatu.

 Wakati idadi hiyo ya mashahidi ikitarajiwa kutoa ushahidi imeelezwa kwamba  upande wa mashtaka unatarajiwa kuwasilisha vielelezo 19.

Leo Agosti 23, mwaka 2021 Mbowe na wenzake ambao ni Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Abdallah Ling'wenya wamesomewa maelezo ya mashahidi hao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.

Jopo la mawakili wa serikali likiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Nassoro Katuga walidai kwamba Agosti 17,mwak  2021 Mahakama ya Mafisadi  ilileta taarifa katika Mahakama Kuu kitengo cha Makosa ya Uhujumu Uchumi walipeleka taarifa katika mahakama ya Kisutu kuwa  Mbowe na wenzake  waletwe mahakamani hapo wasomewe mashtaka yao na maelezo ya mashahidi ili kesi ihamie mahakamani hapo

Kesi hiyo imeitishwa leo chini ya hati ya dharura kwa ajili ya washitakiwa kusomewa maelezo ya mashahidi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo wamesomewa mashtaka saba likiwemo la kula njama ya kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo kumsababishia majeraha Lengai Ole Sabaya  aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya hài.

Baada ya kusomewa maelezo, Hakimu mshitakiwa Halfan Hassan, Adam Kasekwa na Mohammed Lingenya wamekana maelezo hayo yaliyosomwa na upande wa mashitaka, huku Mbowe akisema hana cha kusema ataenda kuyasema Mahakama Kuu.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba amesema kuwa tayari hatua zote ambazo zinatakiwa kufanywa mahakama hiyo tayari zimekamilika, kilichobaki ni Mahakama Kuu kuanza kusikiliza mashahidi.

Mashtaka hayo ni pamoja na kula njama za kutenda ugaidi ambapo Mbowe anatuhumiwa kufadhili vitendo hivyo vya kulipua vituo vya mafuta kwa kutoa zaidi ya shilingi 600,000.

Inadaiwa Mbowe alituma kiasi cha shilingi 600,000 kwa washitakiwa wenzake kwa ajili ya kufanya maandalizi ya vitendo vya ugaidi ikiwemo kutaka kulipua vituo vya mafuta, mikusanyiko ya watu, kukata miti na kuisambaza barabarani.

Piaa watuhumiwa wote wanatuhumiwa kushiriki vikao vya kutenda kosa la ugaidi huku mshtakiwa wa pili anatuhumiwa kumiliki bastola yenye risasi tatu kwa ajili ya kutenda kosa la ugaidi.

Aidha, mshtakiwa wa kwanza anatuhumiwa kumiliki nguo, begi na koti zote za Jeshi la Wananchi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...