Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuondoka nchini kesho tarehe 24 Agosti, 2021  kuelekea nchini Zambia kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Zambia  Mhe. Hakainde Hichilema.

 Sherehe  za Uapisho wa Rais huyo Mteule wa 7 wa Zambia Mhe. Hichilema zitafanyika katika Uwanja wa Taifa wa Mashujaa (National Heroes Stadium), Jijini Lusaka.

 Katika msafara wake Mhe. Rais Samia ataongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Idara ya Oganaizesheni wa CCM Ndugu Maudline Cyrus Castico, Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mhe. Mizengo Peter Pinda, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mzee Kombo Hassan Juma, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mzee Henry Daffa Shekifu, na Mbunge wa Jimbo la Mtera na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mhe. Livingstone Joseph Lusinde.

 Aidha, Rais mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atashiriki katika sherehe hizo akiwa Kiongozi wa timu ya Waangalizi wa Uchaguzi kutoka  Jumuiya ya Madola.

 

Jaffar Haniu

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...