Na Mwandishi wetu, Babati
MKAZI
wa Kijiji cha Garanja, Kata ya Tlawi, Wilayani Mbulu, Mkoani Manyara,
Maria Suruhu (56) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua kwa
kumpiga kichwani na shoka mume wake Lego Kerehemi (54).
Kamanda
wa polisi wa mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi (ACP) Marrison Mwakyoma
akizungumza jana amesema tukio hilo limetokea kwenye kata hiyo ya
Tlawi.
Kamanda Mwakyoma
amesema chanzo cha kifo ni ugomvi wa ndani baada ya mwanamke huyo
kuulizwa alipochelewa baada ya wote kutoka kunywa pombe kilabuni.
Amesema mume na mke walienda kilabuni kunywa pombe na walipomaliza waliamua kurudi nyumbani huku wakiongozana wawili barabara.
"Baadaye
waliachana njiani kila mmoja akafuata njia yake ila kufika nyumbani
mume akawahi kufika na mke akachelewa kidogo," amesema kamanda Mwakyoma.
Amesema mume akamuuliza mkewe kwa nini amechelewa kurudi muda wote huo na ndipo akaanza kumpiga kwa kosa hilo.
"Wakati
wakiendelea kupigana mke alichukua shoka na kumpiga nalo kichwani mume
wake na kusababisha kifo chake papo hapo," amesema kamanda Mwakyoma.
Amesema
mwanamke huyo Suruhu anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji hayo
na anatarakiwa kufikishwa mahakamani pindi uchunguzi ukikamilika.
Mkazi
wa eneo hilo, Julius Slaa amesema hivi sasa watoto wa familia hiyo
wamepata pigo kubwa kutokana na tukio hilo kwani ni sawa na kuwapoteza
wazazi wote wawili.
"Baba
amefariki dunia kwa kuuawa na mama ambaye hivi sasa yupo mahabusu
kutokana na ulevi wao hatima ya watoto itakuwa mbaya," amesema.
Kamanda wa polisi wa Mkoa Manyara, Kamishina Msaidizi (ACP) Marrison Mwakyoma (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...