Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
WILAYA
ya Kibaha imemkabidhi ,kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ,LT.Josephine
Mwambashi ,madawati 50 kisha kuyakabidhi kwa halmashauri ya Mji wa
Kibaha wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha.
Akikabidhiwa
madawati hayo wakati wa uzinduzi wa madarasa matano katika shule ya
msingi Mtongani ,wilayani Kibaha ,alisema ni muhimu kujenga na kuboresha
mazingira bora kwa wanafunzi ili waweze kujiinua kitaaluma.
Kutokana
na hilo , Mwambashi aliwaelekeza ,watendaji wanaopewa dhamana ya
kusimamia miradi mbalimbali ya kimaendeleo kuwa wazalendo,ili miradi
hiyo itoe huduma katika jamii.
"Nimejiridhisha ,tumejiridhisha vizuri na kuona nyaraka za malipo, hivyo nazindua madarasa haya"alifafanua Mwambashi .
Wakati huo huo , Mwambashi aliwaasa wanafunzi kuacha matumizi mabaya ya TEHAMA kwa kuangalia vitu visivyo na maadili kwao.
Awali
Mkuu wa wilaya ya Kibaha , Msafiri alibainisha ,walipata milioni 24
kutoka kwa wadau wa elimu ambapo milioni 7 walitenga na kununua madawati
50 ambayo yamegawanywa 25 Mji wa Kibaha na 25 mengine Kibaha Vijijini.
Mbio
za mwenge pia zimekagua mradi wa shamba la mikorosho KJ 832 Ruvu
,lilianzishwa mwaka 2018 ,lina ukubwa wa hekari 115 na limegharimu
milioni 36 .
Akielezea mradi huo,meneja wa shamba hilo ,Lugomola Kifusi anasema, kwa msimu huvuna tani 1.5.
Mwenge huo ukiwa wilayani Kibaha utakimbizwa katika miradi 13 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 2.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...