Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
HATIMAYE!!! Nyota ghali wa Kimataifa wa Argentina, Lionel Messi (34) ameweka wino wa mkataba wa miaka miwili na uwezekano wa kuongeza mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya £25m kwa mwaka kuitumikia Klabu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa baada ya siku za hivi karibuni kutangazwa kuachana na Klabu yake ya tangu utotoni FC Barcelona.
Messi amesaini mkataba huo wa miaka miwili na PSG huku akitajwa kulipwa kiasi cha mshahara wa €35m (£29.6m) klabuni hapo, sambamba na kupewa Jezi namba 30! namba ambayo haikutegemewa na mtu yoyote kupewa Nyota huyo aliyegusa nyoyo, hisia za wengi ulimwenguni kuondoka kwake Barca. Wengi walidhani huenda Messi atapewa kuvaa Jezi namba 10.
Messi amepewa Jezi namba 30 na PSG, Jezi ambayo alianza nayo mwaka 2003 katika Klabu yake ya zamani ya Barcelona.
Vyombo mbalimbali vya Habari ulimwenguni tayari leo Agosti 11, 2021 vimeripoti usajili huo ambao huenda unaweza kuwa umevunja rekodi ya usajili duniani ukilinganisha na sajili nyingine za Wachezaji ulimwenguni.
Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa PSG, Nasser Al-Khelaïfi amesema “tunaamini Nyota huyo (Messi) ameichagua PSG na tunamkaribisha kwa moyo mmoja katika familia yetu. Tunaamini matamanio yake kuendelea kuwa katika ubora wa hali ya juu na kushinda mataji mengi, na malengo yetu sisi PSG siku zote ni kufanya hivyo”.
Kufuatia kukamilika kwa dili hilo, Lionel Messi sasa ataungana na Wachezaji wengine maarufu ulimwenguni kusakata kabumbu, kina Neymar Jr, Angel Di Maria, Kylian Mbappe, Mauro Icardi, Achraf Hakimi, Keylor Navas, Kimpembe, Marco Verratti, Sergio Ramos na wengine wengi wanaosuka Kikosi hicho cha matajiri wa Ufaransa.
Kikosi hicho cha Kocha Mkuu, Mauricio Pochettino huenda misimu ijayo kikafanya makubwa kwenye mashindano mbalimbali kutokana na kuundwa na Wachezaji wengi maarufu na ghali duniani kulinganisha timu nyingine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...