Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar akihutubia katika kongamano la wahasibu wanawake wa Tanzania TAWCA linaloendelea katika Hotel Verde visiwani Zanzibar.
WANAWAKE Wahasibu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wameshiriki kongamano la kitaaluma la wanawake wahasibu linalofanyika katika hotel ya Verde Zanzibar.
Kongamano hilo la nne limefunguliwa Agosti 19, 2021 na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdallah akimwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ally Hassan Mwinyi.
TANESCO imefadhili kongamano hilo lengo likiwa ni kuwakutanisha wahasabu wanawake wa TANESCO na wataalamu wengine wa kada hiyo kutokana na makongamano kuwa sehemu mahususi ya kuzungumzia masuala ya kada ya husika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...