Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Kiungo wa Kimataifa wa Zambia na Klabu ya Simba, Clatous Chota Chama amefunguka kwa mara ya kwanza tangu kutokea sintofahamu baina yake yeye, Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu hiyo, Mohammed Dewji na mashabiki wa Soka Tanzania.
Sintofahamu hiyo ilitokea baada ya Mchezaji huyo kuwaalika mashabiki zake kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram (Insta Live) kuwapa nafasi mashabiki hao kuuliza maswali na yeye kutoa majibu ya papo kwa hapo.
Wakati akizungumza na mashabiki hao imeelezwa kuwa Chama alimuongelea aliyekuwa Msemaji wa Klabu hiyo, Haji Manara ambaye kwa sasa hayupo katika nafasi hiyo baada ya kutofautiana na Uongozi wa Klabu.
Pia wakati Chama anajibu maswali ya mashabiki hao, Mwekezaji wa Klabu, MO Dewji aliingia katika ‘Insta Live’ hiyo na kumshutumu Chama baada ya kumuongelea Haji Manara ambaye ameachana na Klabu katika nafasi yake ya Usemaji.
Kupitia Mitandao yake ya Kijamii, Clatous Chama amefunguka kuhusu sintofahamu hiyo na kuweka sawa suala hilo kutokana na mkataba wake wa kuendelea kuitumikia Klabu ya Simba sambamba na kujenga amani, umoja na mshikamano ndani ya Klabu hiyo.
Chama ameandika, “Jana ilitokea sintofahamu lakini yote kwa yote ni sawa tu. Nasema binafsi naheshimu kila mtu katika Klabu ya Simba bila ubaguzi na shinikizo”.“Wengi wanapenda tugombane bila sababu, tusiwape nafasi maadui watugombanishe”.
Tuna kazi ya kutetea Ubingwa wetu wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho (ASFC) msimu ujao sambamba na kumalizia malengo yetu katika Ligi ya Mabingwa ya Afrika (CAF CL)”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...