Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Mkuu
wa mkoa wa Pwani, Aboubakar Kunenge ,ameshiriki kwenye Mazishi ya
Watoto watano waliofikwa na mauti kwenye Ajali iliyohusisha Pikipiki na
Fuso Eneo la Kata ya Kimange Halmashauri ya Chalinze.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa ameeleza kuwa Mnamo Tarehe 6
Agosti, 2021 majira ya saa 1 :15 Jioni Gari aina Mitusubish Fuso Na 198
CWN ikitokea Dar es salaam kwenda Arusha iligonga Mwendesha Pikipiki
kusababisha vifo vya Wanafunzi wanne pale pale na mmoja kufariki
akipatiwa matibabu Hospital ya Jeshi Kihangaiko.
Alieleza
kuwa Wanafunzi hao watano wa Kimange Sekondari walikuwa wamepakiana
kwenye Pikipiki wakitokea Kimange kuelekea Mbwewe. Wanafunzi hao
walikuwa wakitokea michezoni shule Jirani ya kwamakocho Sekondari.
Wanafunzi
hao waliofariki ni Laya Ubwa Masudi (16) mwanafunzi wa kimange
Sekondari Kidato cha tatu, Furaha Athumani (16) Mwanafunzi Kimange
Sekondari Kidato cha tatu, Athumani Bushiri (15) Mwanafunzi kimange
Sekondari Kidato cha Kwanza, Amina Msomba (15) Mwanafunzi Kimange
Sekondari Kidato cha Kwanza na Athumani Mchafu (17) Mwanafunzi Kidato
cha tatu.
Ameeleza kuwa Chanzo cha Ajali hiyo ni
Uzembe wa Dereva wa Gari na mwendo kasi uliosababisha kushindwa kumudu
Gari hilo na kupelekea kumgonga Mwendesha Pikipiki akiyekuwa mbele
yake.
Alithibitisha kuwa Jeshi la polisi limefanikiwa kumshikilia Dereva wa Gari hilo kwa ajili ya hatua za kisheria,
Kunenge
alitoa pole kwa Familia na Wananchi wa Kata hiyo kwa Msiba Mkubwa
ambao wameupata. "Kwa niaba ya Mhe Rais Mhe. samia Suluhu Hassan nitoe
pole nyingi kwenu alisema Kunenge"
"Kubwa zaidi kwetu ilikuwa ni kuja kushiriki nanyi, tumekuja na Swadaka Ndogo kwa ajili ya kufariji familia hizi.
"Yaliyotokea
yametokea, niwaombe tuzingatia matumizi ya vyombo vya Moto. Sisi kwa
upande wa Serikali tunaendelea kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria za
Nchi. Dereva wa Gari hilo tunaye tutachukua hatua" Alisema Kunenge.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...