NA YEREMIAS NGERANGERA…..NAMTUMBO

Timu ya wataalamu wa afya  ikiongozwa na  mganga mkuu wa wilaya ya Namtumbo Lucia Kafumu wanatoa elimu kwa wananchi  wa kata na vijiji vya wilaya ya Namtumbo   kuhusu umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19 na kufanikiwa kuchanja wananchi 932 kwa siku mbili kwa siku ya  jumatatu na jumanne ya wiki hii.

Wananchi wa kata ya Likuyu ,kata ya Mgombasi,kata ya kitanda walipatiwa elimu ya ugonjwa wa UVIKO19  kwa kuelezwa nini maana ya ugonjwa huo,dalili za ugonjwa huo ,chanzo cha ugonjwa  pamoja na kuelezwa njia sahihi ya kuzuia ugonjwa  usilete madhara makubwa kwa wananchi ni kupata chanjo ya UVIKO 19 ambapo wananchi katika kata hizo waliojitokeza kusikiliza elimu kutoka kwa wataalamu wa afya na kukubali kupata chanjo ya UVIKO19.

Kata ya Mgombasi Kijiji cha Nambecha kitongoji  cha masimango pekee kilichanja wananchi 74 wote waliohudhuria mkutano huo  Kijiji cha  mandela  Kilichanja wananchi 63 na Kijiji cha Likuyuseka kilichanja wananchi 50 siku ya kwanza huku wananchi wengine wakidai utaratibu huo uendelee kwa kuwa wananchi wengi hawana uwezo wa kusafiri umbali mrefu wa kufuata huduma ya chanjo katika vituo vilivyotengwa na serikali.

Saidi Hashimu mkazi wa Kijiji cha Mandela alihoji wataalamu wa afya  sababu ya Watoto chini ya miaka 18 kutochanjwa huku wazazi wake wakihimizwa kuchanjwa na kuwataka wataalamu kumpatia majibu ambayo yanawafanya Watoto hao kutochanjwa.

Kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Godwin Luta pamoja na mambo mengine alimthibitishia bwana Saidi Hashimu kuwa kinga za Watoto waliochini ya miaka 18 ni  thabiti na zenye uwezo wa kupambana na virusi kuliko kinga za watu wenye umri Zaidi ya miaka18.

Naye Amina Ngonyani mkazi  wa  Kijiji cha Mtonya alihoji mtu mwenye magonjwa mengine kama kisukari,BP,UKIMWI na mengineyo hawezi kusumbuliwa baada ya kuchoma chanjo hiyo aliuliza Amina kwa kaimu mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Luta ambaye alimjibu hawezi kusumbuliwa na kumtaka kuchukua namba yake ya simu ampigie simu kama atajisikia tofauti alisema Luta.

Timu ya wataalamu wa afya wilaya ya Namtumbo wanaendelea na kuhamasisha wananchi katika kata na vijiji kutoa elimu  katika kata zote 21 za wilaya ya Namtumbo kwa kuwahamasisha wananchi hao kuchanja  ili  waweze kujikinga na UVIKO19 ambapo kwa siku mbili timu hiyo ya wataalamu wa afya wamechanja wananchi 932 katika wilaya ya Namtumbo



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...