NA TIGANYA VINCENT

MKUU wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ametoa elimu kwa wakazi wa Kijiji cha Mwisole wilayani Uyui kuhusu umuhimu wa kupata chanjo ya UVIKO 19 na kufanya watu kujitokeza na kupata chanjo katika eneo la Mnada wa Mwisole.


Dkt. Batilda ameendesha zoezi hilo leo ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kufikisha elimu kwa wananchi wengi ambao bado hawana uelewa sahihi wa faida ya chanjo ya UVIKO 19.

Amesema viongozi wa Kitaifa wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wameshachanja na wale wa Mkoa wa Tabora na wameshachanjwa na hakuna madhara yoyote waliyopata.

Dkt. Batilda chanjo hiyo salama na inatolewa bure kwa mwananchi yoyote ambayo umri wake unazidi miaka 18 .

“Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan anatupenda sana na ndio maana ametuletea chanjo kwa ajili ya kupambana na ugonjwa UVIKO 19 ambao ni hatari sana …ni vema kwa wale ambao hawajachanjwa wakachangamkia fursa hiyo…na hivi sasa hatuki mfuate chanjo mbali tunawaletea huku mlipo” amesisitiza

Dkt. Batilda amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan inajari sana afya za wananchi wake na ndio maana inajenga miundombinu mbalimbali ambao kwa Mkoa wa Tabora imetoa fedha kwa ajili ya kuongeza Vituo vya Afya vipya viwili.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa huyo amewakumbusha wakazi wa Tabora kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya UVIKO 19 kwa kuepuka misongamano,kunawa na maji tiririka na kuvaa barakoa.




Mhudumu wa Afya Kutoka Hospitali ya Wilaya ya Uyui Rahel Mazinge akitoa chanjo ya kujikinga na UVIKO 19 kwa wakazi wa Kijiji cha Mwisole walikuwa katika Mnada wa kila Jumatano.





Mkuu wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (mwenye kipaza sauti) akitoa elimu ya faida ya chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO 19 leo wakati ziara yake katika Mnada uliopo katika Kijiji cha Mwisole wilayani Uyui.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (kushoto) akibadilisha mawazo leo na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Kisare Makori(kulia) mara baada ya kumalizika kwa utoaji wa elimu ya umuhimu wa chano ya UVIKO 19 katika mnada uliopo katika Kijiji cha Mwishole.
Picha na Tiganya Vincent

 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...