Na Mwandishiwetu,Mbeya
Asilimia 50 ya wanawake nchini wamenufaika na mikopo ya Zaidi ya Sh 600 Bilioni ,kupitia Benki ya Biashara Tanzania,(TCB)tangu Serikali ilipoingia ubia.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo ,Sabasaba Moshingi ,amesema leo Septemba ,24,2021, mkoao hapa kwenye kongamano la wanawake lililoandaliwa na benki hiyo na kuhudhuriwa na Naibu Spika na Mbunge wa jimbo la Mbeya ,Dkt Tulia Ackson.
Amesema kuwa mikopo hiyo imekuwa mkombozi mkubwa kwa wanawake jambo ambalo limeleta tija ya kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa lengo la kutekeleza maagizo ya serikali kuwezesha wanawake.
“Asilimia 83 ya benki hiyo inamilikiwa na Serikali ya Tanzania na Zanz'bar hivyo imelenga zaidi kuwezesha wanawake kiuchumo hivyo ni vyema sasa kutumia fursa za mikopo kupitia benki hiyo ili kuboresha miradi mbalimbali ya maendeleo"amesema.
Kwa upande wake Naibu Spika Dkt ,Tulia Ackson ameziagiza taasisi za kifedha kufanya tathimini za miradi inayofanywa na wanawake kabla ya kuwapatia mikopo jambo ambalo uchangia mali zao kutaifishwa.
Amesema kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa ya wakopaji kukwama kurejesha mikopo na sababu kubwa ni kutokuwa wabunifu na kuchukua mikopo mikubwa isiyoendana na biashara walizonazo.
Mfanyabishara wa duka la Jumla ,Zainab Ally amesema kuwa tangu kuwepo kwa mifumo ya utoaji mikopo kwa wanawake imekuwa chachu ya kuwainua kiuchumi na kuachana na utegemezi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...