MKUU wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga Halima Bulembo amewataka wafanyabiashara wanaowaajiri watoto wenye umri wa kwenda shule kuacha mara moja vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akipita kukagua na kuangalia changamoto zilizopo kwenye masoko matano yaliopo Muheza na stend kuu ya mabasi ya wilaya hiyo.

Bulembo amesema Serikali ya Awamu ya sita inafanya kazi kubwa kuwekeza katika elimu bila malipo , hivyo haiwezi kukaa kimya kuangalia mfanyabiashara anakatisha ndoto za watoto hao kwa kuwaajili kufanya biashara ndogondogo

" Ni marufuku kuwafanyisha watoto biashara ndogondogo za kuuza karanga na biashara zingine sababu kufanya hivo ni kosa kisheria na hata sheria ya mtoto inakataza mtoto kutumikishwa,"amesema Bulembo.

Mkuu wa wilaya huyo amesema watoto wote wanatakiwa kupelekwa shule kupata elimu ili ije iwasaidie katika maisha yao ya badae.

Wakati huo huo Bulembo ametumia fursa hiyo kupita katika masoko hayo ili kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu na Waziri Mkuu lilowataka kuangalia namna bora ya kuwatengea maneno wamachinga.

Lengo likiwa waweze kufanya biashara zao ambapo alikutana na changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu wa miundombinu ya soko ,umeme na maji ambayo vilipatiwa ufumbuzi palepale .

Suala lingine lililojitokeza ni kutorasimishwa kwa baadhi ya masoko ambayo Rais ameagiza masoko ya namna hiyo yarasmishwe ili wapewe wamachinga maeneo ambayo tayari yamerasimishwa.

"Mwezi Mmoja tuliopewa sisi kama wilaya tutahakikisha tunatenga maeno bora kwa wamachinga ili waweze kufanya biashara zao bila kubughuziwa,"amesema Bulembo

Aidha ameiagiza halmashauri ndani mwezi mmoja wahakikishe wanamaliza changamoto zote zilizopo ili kuweka mazingira safi kwa wafanyabiashara wanautumia masoko hayo.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...