Miradi miwili inayotekelezwa na DAWASA kuwa mwarobaini wa changamoto za upatikanaji wa maji katika jimbo la Kibamba katika Manispaa ya Ubungo mkoa wa Dar es Salaam. Miradi hiyo ni mradi wa wa Maji wa King’azi A na B pamoja na mradi wa Usambazaji  Maji wa Kibesa.

Akizungumza wakati wa utoaji wa taarifa ya miradi hiyo Mkurugenzi wa Biashara na Huduma kwa Wateja DAWASA, Bi Rithamary Lwabulinda amesema kuwa DAWASA wamejipanga kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo hadi pale itakapokamilika. Pamoja na kuomba wananchi kuwa walinzi wakati na baada ya kumalizika kwa miradi hiyo.

Amesema mradi wa maji wa King’azi A na King’azi B utatekelezwa kwa umbali wa Kilomita 12 ukihusisha ulazwaji wa Bomba Kuu na za usambazaji katika mitaa mbalimbali ya King’azi na Viunga Vyake. Pia amesema Mradi huo utanufasiha wakazi wa maeneo ya King’azi A, King’azi B, Kifuru, Msigwa na Sehemu ya wakazi wa eneo la Hali ya hewa na utaweza kuwahudumia wateja zaidi ya 2000.

Pia amesema katika mradi wa maji wa Kibesa utaotekelezwa na DAWASA kwa mapato ya ndani utatekelezwa kuanzia tenki kubwa la Kuhifadhi na kusambaza maji Malolo hadi Mpiji Cente kupitia kijiji cha Kibesa.

"Mradi huo  utahusisha ujenzi wa Mabomba madogo na makubwa ya kusambazia maji ubali wa kilomita 8.2 na mradi huu utaweza kunufaisha wateja zaidi ya 1630. Pia amesema Wanufaika wa mradi huo ni Kiwanda cha Mboji, Kijiji cha Kibesa na baadhi ya maeneo ya Mpiji Center." alisema Lwabulinda.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kibamba Issa Mtemvu amewashukuru DAWASA kwa kuweza kuja na mwarobaini wa kero ya maji katika jimbo la Kibamba yakiwemo maeneo ya maeneo ya King’azi A, King’azi B, Kifuru, Msigwa ,  Sehemu ya wakazi wa eneo la Hali ya hewa, Kijiji cha Kibesa na baadhi ya maeneo ya Mpiji Center ambapo upatikanaji wa maji niwa shida.

Pia amewasitiza DAWASA kufanya kazi ili kuweza kutatua changamoto za maji wa wananchi na kufikia lengo la kumtua mama ndoo kichwani na kuwataka wananchi kuwa watulivu wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo miwili itakayoweza kuondoa tatizo la upatikanaji wa maji katika jimbo la Kibamba.

Mkurugenzi wa Biashara na Huduma kwa Wateja DAWASA, Bi Rithamary Lwabulinda akikabidhi mabomba ya Maji kwa Mbunge wa Kibamba, Issa Mtemvu kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji kwenye mitaa ya King'azi A na B, Kifuru na Kilimahewa. Kukamilika kwa mradi huo kutawezesha kaya zaidi ya 2000 kupata huduma ya Majisafi. 
Mkurugenzi wa Biashara na Huduma kwa Wateja DAWASA, Bi Rithamary Lwabulinda akisoma utekelezaji wa mradi wakati wa  kukabidhi mabomba ya Maji kwa Mbunge wa Kibamba, Issa Mtemvu kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji kwenye mitaa ya Kingazi A na B, Kifuru na Kilimahewa. Kukamilika kwa mradi huo kutawezesha kaya zaidi ya 2000 kupata huduma ya Majisafi.
Mbunge wa Jimbo la Kibamba Issa Mtemvu akizungumza na wananchi wa Mtaa wa King'azi A pamoja na wafanyakazi wa DAWASA wakati wa kupokea mambomba ya maji yatakayotandazwa katika mtaa wa King'azi A na B utakaohudumia ingazi A na B, Kifuru na Kilimahewa. Kukamilika kwa mradi huo kutawezesha kaya zaidi ya 2000 kupata huduma ya Majisafi.
Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA  Kinyerezi, Barton Mwalupasu akizungumza jambo pamoja na kumkaribisha Mkurugenzi wa Biashara na Huduma kwa Wateja DAWASA, Bi Rithamary Lwabulindakwa ajili ya kutoa taarifa ya mradi wakati wa  kukabidhi mabomba kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji kwenye mitaa ya Kingazi A na B, Kifuru na Kilimahewa. Kukamilika kwa mradi huo kutawezesha kaya zaidi ya 2000 kupata huduma ya Majisafi.
Wananchi wakifuatilia makabidhiano ya mabomba kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji kwenye mitaa ya King'azi A na B, Kifuru na Kilimahewa. Kukamilika kwa mradi huo kutawezesha kaya zaidi ya 2000 kupata huduma ya Majisafi. 
Mkurugenzi wa Biashara na Huduma kwa Wateja DAWASA, Bi Rithamary Lwabulinda akiwa kwenye picha ya pamoja na Mbunge wa Kibamba, Mheshimiwa Issa Mtemvu pamoja na viongozi wa Mtaa wa King'azi A baada ya kumaliza kukabidhi mambomba ya mradi wa maji utawezesha kaya zaidi ya 2000 kupata huduma ya Majisafi
Baadhi ya mabomba yaliyofika kwenye utekelezaji wa mradi wa maji kwenye mitaa ya King'azi A na B, Kifuru na Kilimahewa.
Wananchi wa Mtaa wa Kibesa wakishangilia mara baada ya gari lililobeba mambomba kuwasili kwenye eneo ilo kwa ajili ya mradi wa Usambazaji maji wa Kibesa utakaowezesha kupatikana kwa huduma ya Majisafi kwenye kaya 1630.
Meneja wa Mkoa wa Kihuduma DAWASA Mabwepande, Harouna Taratibu akizungumza jambo pamoja na kumkaribisha Mkurugenzi wa Biashara na Huduma kwa Wateja DAWASA, Bi Rithamary Lwabulinda  kwa ajili ya kutoa taarifa ya mradi wa mradi wa Usambazaji maji wa Kibesa utakaowezesha kupatikana kwa huduma ya Majisafi kwenye kaya 1630.
Mkurugenzi wa Biashara na Huduma kwa Wateja DAWASA, Bi Rithamary Lwabulinda akisoma utekelezaji wa mradi wakati wa  kukabidhi mabomba ya Maji kwa Mbunge wa Kibamba, Mheshimiwa Issa Mtemvu kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Usambazaji maji wa Kibesa utakaowezesha kupatikana kwa huduma ya Majisafi kwenye kaya 1630.
Mbunge wa Jimbo la Kibamba Issa Mtemvu akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Kibesa pamoja na wafanyakazi wa DAWASA  wakati wa kukabidiwa mabomba kwa ajili ya mradi wa Usambazaji maji wa Kibesa utakaowezesha kutoa huduma ya Majisafi kwenye kaya zaidi ya 1630.
Mkurugenzi wa Biashara na Huduma kwa Wateja DAWASA, Bi Rithamary Lwabulinda akikabidhi mabomba ya Maji kwa Mbunge wa Kibamba, Mheshimiwa Issa Mtemvu kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji wa Usambazaji maji wa Kibesa utakaowezesha kupatikana kwa huduma ya Majisafi kwenye kaya 1630.
Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Kibesa wakifuatilia makabidhiano ya mabomba kwa ajili ya  utekelezaji wa mradi wa maji wa Usambazaji maji wa Kibesa utakaowezesha kupatikana kwa huduma ya Majisafi kwenye kaya 1630.

Mbunge wa Kibamba, Mheshimiwa Issa Mtemvu akifurahia na wananchi wa mtaa wa Kibesa mara baada ya kupokea mabomba ya mradi wa maji wa Usambazaji maji wa Kibesa utakaowezesha kupatikana kwa huduma ya Majisafi kwenye kaya 1630
Wananchi wa kiyapokea mabomba kwa ajili ya mradi wa maji wa Usambazaji maji wa Kibesa

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...