MBUNGE wa Jimbo la Hanang mkoani Manyara Mhandisi Samwel Hayuma amewataka wazazi na walezi kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha wanafunzi wanakula chakula cha mchana shuleni .
Hayuma ametoa Kauli hiyo wakati wa mahafali ya 22 katika shule ya msingi Bassotughang iliyopo Kata ya Hidet Wilayani humo ambapo amesema wazazi na walezi wa shule hiyo pamoja na shule nyingine wilayani hapo wanapaswa kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa wanafunzi hao kwani serikali imeshatekeleza wajibu wake kupitia elimu bila malipo.
Amesema wanafunzi wanapokuwa wanakula shuleni kiwango cha taaluma huongezeka.
Amesema, mpango wa utoaji wa chakula Shuleni ambao wazazi hutakiwa kuchangia kwa mujibu wa sera ya Elimu pasipo malipo, husaidia kuleta usawa kati ya walionacho na wasionacho, kuimarisha mahudhurio na kutunza muda wa ratiba za shule na kusisitiza kuwa endapo mambo haya yote yatafanyika kiusahihi yanamchango mkubwa kwa wanafunzi kufanya vizuri darasani.
Hata hivyo ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika shule hiyo katika kuboreha miundombinu yake kwani naye alisoma hapo elimu yake ya msingi mwaka 1990.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...