Kamati
ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI, Kifua Kikuu, Dawa za Kulevya na Magonjwa
yasiyoambukiza imeupongeza mkoa wa Rukwa kwa mafanikio iliyoyapata
katika kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI ambapo mkoa una
maambukizi ya asilimia 4.4 chini ya kiwango cha kitaifa cha 4.7
Pongezi
hizo zimetolewa leo (27.09.2021) na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe.
Fatma Hassan Toufiq (Mb) wakati wa kikao na viongozi na watumishi wa
serikali na wadau mjini Sumbawanga.
Akitoa
taarifa ya mkoa ,Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu
alisema mkoa una watu 34,000 wanaoishi na VVU/UKIMWI ambapo kati yao
28,000 sawa na asilimia 95 wametambuliwa na wanapata huduma za tiba na
dawa za kupunguza makali ya VVU
Kuhusu
huduma za tohara kwa hiari, Dkt. Kasululu alisema wanaume 34,549 kati
ya lengo la watu 35,999 wamepatiwa huduma hiyo kwenye mkoa huo ikiwa ni
makakati wa kupungunza maambuzi ya VVU/Ukimwi.
Naye
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Jaqueline Msongozi (Mb)
akizungumza kwenye kikao hicho alitoa rai kwa wanawake kote nchini
kutokubali kuwa na mahusiano ya kingono na wananume amabao hawajafanyiwa
tohara ili kuondoa hatai ya kupata magonjwa.
"
Niwashauri wanawake wenzangu wa Rukwa na kote nchini kabla ya kuwa na
mahusiano ni vizuri kujua endapo mwanaume amepata tohara au la .Ukikuta
hajapata tohara basi usitoe huduma" alisema Mhe. Msongozi.
Kwa
upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Denis Bandisa amesema
anashukuru kwa waheshimiwa wabunge hao kupata nafasi ya kutembelea mkoa
wa Rukwa kujionea hali ya utoaji huduma za afya kwenye masuala ya UKIMWI
na magonjwa mengine.
Bandisa
ameihakikishia kamati hiyo kuwa maeleokezo na ushauri watakao utoa
wakati wa ziara yao ya siku mbili mkoani Rukwa yatafanyiwa kazi na
mrejesho utatolewa kwa Bunge.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya
UKIMWI,Kifua Kikuu, Dawa za Kulevya na Magonjwa yasioambukiza Mhe. Fatma
Hassan Toufiq akiongoza kikao na viongozi na wadau wa mkoa wa Rukwa leo
mjini Sumbawanga.Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Boniface Kasululu akitoa taarifa ya mkoa kuhusu mapambano dhidi ya UKIMWI,Kifua Kikuu na magonjwa yasiyoambukiza leo wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge mjini Sumbawanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...