Na Linda Shebby ,Kibaha
WANAWAKE
wa Mkoa wa Pwani wamepewa wito wa kujitokeza kwa wingi katika
kongamano la Fursa Gala ambalo limepangwa kufanyika Oktoba 3 mwaka
huu kwenye ukumbi wa Destiny uliopo Kwa Mathias Kibaha Mkoani Pwani
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Kampuni ya
Herochic ambayo ndiyo waandaaji Bi Suzana Mdonya alisema kuwa
kongamano hilo lina lengo la kumkomboa mwanamke kiuchumi ambapo pia
wanatarajia kuwa litawakutanisha wanawake kutoka katika Kanda ya
Pwani na viunga vyake ikiwemo Mkuranga, Kibaha, Chalinze na Mlan na
kuwawezesha kujifunza njia sahihi za biashara na uwekezaji kutoka
kw a wakufunzi mahiri nchini na kuwawezesha wanawake kuwa na
nidhamu ya mtaji wa biashara na fedha kwa ujumla ambazo wanazipata
katika kila nyanja ya ujasiriamali waoufanya.
"Tunakwenda
kumwezesha mwanamke Ili aweze kutambua thamani ya mtaji wake wa
biashara na kumpatia elimu na mbinu mbadala ya kuweza kukuza mtaji
wake pamoja na kukua kibiashara huku lengo likiwa kumkomboa mwanamke
kiuchumi" alisema Suzana
Aidha kuwa kauli mbiu ya kongamano hilo
ni ' Uwezo wa Mwanamke' ambapo pia katika Fursa Gala litawakutanisha
wajasiriamali wakubwa na wadogo, wamiliki wa Viwanda huku lengo likiwa
ni kupeana masoko ya biashara, kuongeza wigo wa kupata masoko kwa
wajasiriamali.
Suzana anakitaja kiingilio kwenye kongamano hilo kuwa ni 30,000 & 50,000 (VIP)
Akielezea
kuhusu Herochic alisema kuwa ni Kampuni binafsi katika kutekeleza
majukumu ya kijamii ambapo imeandaa kongamano hilo kwa kushirikiana na
Vitenge na Tamrah Kibaha, HEROCHIC inayojishughulisha na Ubunifu na
ushonaji wa sare za maofisi pamoja na Suti za kiume na kike.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...