Na Editha Karlo,Kasulu.
BARAZA la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) wanashiriki maonyesho ya tatu ya shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO)ambayo kitaifa yanafanyika Mkoani Kigoma Wilayani Kasulu.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho hayo kwenye banda lao Mkurugenzi mkuu wa Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira(NEMC),Dkt. Samwel Gwamaka alisema kuwa kuna wajasiliamali wachache wamekuwa wakifanya shughuli zao bila kuangalia athari za mazingira katika shughuli zao wanazofanya.
Alisema NEMC wamekuwa wakitoa elimu ya mazingira kwa wajasiliamali wadogo ili waweze kulinda mazingira wanapokuwa kwenye maeneo yao ya kazi.
"Suala la utunzaji wa mazingira linapaswa kuwa ni suala ya maisha yetu ya kila siku,tupo hapa kwenye maonesho haya ya SIDO kwaajili ya kutoa elimu kwa wajasiliamali juu ya kutunza mazingira ili uwekezaji wao wanaoufanya usiwe na athari yoyote kimazingira"alisema
Naye Meneja wa baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) Benjamin Dotto alisema kuwa kwenye banda lao katika kipindi chote cha maonyesho watakuwa wakiwapatia wajasiliamali elimu ya utunzaji wa mazingira.
"Wajasiriamali wote waliopo hapa kwenye haya maonyesho pamoja na wananchi wafike kwenye banda letu hapa wapate elimu ya utunzaji na kuhifadhi mazingira.
Mfanyabiashara Antony Bulindu kutoka Mkoa wa Tabora amelishukuru Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) kwa elimu wanayowapatia juu ya kutunza mazingira katika biashara zao,pia ameishukuru SIDO kwa kuandaa maonyesho hayo ambayo yamewakutanisha wajasilimali na wadau mbalimbali wa sekta ya ukuzaji wa biashara ndogondogo.
Maonesho hayo yameanza tarehe 22 Octoba mwaka huu na kufunguliwa na Makamu wa Rais Dk Philipo Isdor Mpango ambapo yatahitimishwa tarehe 30 mwezi huu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...