Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU
 wa mkoa wa Pwani , Aboubakari Kunenge ,ametoa onyo kwa baadhi ya 
mabaraza ya ardhi mizigo ,ambapo amedai mabaraza hayo yatapimwa kwa kazi
 zao na hatosita kuyavunja yale mabaraza yasiyowajibika.
Kunenge amesema amejipanga kuyasafisha mabaraza yasiyofanya kazi zake ipasavyo na yanayopindisha sheria na kutotenda haki.
Akitoa
 taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ( 
2020-2025), katika mkutano wa halmashauri Kuu ya CCM mkoa ,Kunenge 
alisema , wajumbe wasiotimiza wajibu wao bila kutenda haki wanaondoa 
imani kwa wananchi.
Hata 
hivyo alisema ,wajumbe wa mabaraza hayo wapo kwa ajili ya kutatua 
migogoro haiwezekani, walengwa kwenda mkoa wakati mabaraza hayo yapo ,na
 Kama wapo mizigo waondolewe.
Pia
 Kunenge alifafanua ,wapo watu wanaokwamisha maendeleo kwa  kupitia 
mwamvuli wa chama ,na ameomba wasaidiane na chama kuchukua hatua kwa 
watu hao.
"Migogoro ya wakulima na wafugaji, migogoro ya ardhi inakuwa mingi kutokana na kutofuata sheria"alisisitiza.
Katika hatua nyingine,mkuu wa mkoa huyo alisema migogoro ya ardhi ni muiba katika mkoa huo ,Ni changamoto inayomnyima usingizi .
Kunenge
 alieleza utekelezaji upo vizuri kwa sekta zote na changamoto zilizopo 
serikali inaendelea kuchukua hatua kuboresha na kutatua.
Nae Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani,Ramadhani Maneno alieleza wapo kwenye mahusiano mazuri na serikali Mkoa .
Maneno
 pia aliipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia 
Suluhu,kwa maendeleo ya mkoa huo na kusema wataendelea kumuunga mkono.
Akizungumzia
 masuala ya chanjo ya Uviko 19 ,mganga mkuu wa mkoa wa Pwani,Dokta 
Gunini Kamba alisema zaidi ya watu 15,000 wameshachanja mkoani Pwani.
Gunini
 alieleza , hali ni ya kuridhisha licha ya kuomba wananchi wakachanje 
kwa hiari yao kwani chanjo hiyo inasaidia na haina madhara yoyote.
"Tumekuja
 kuongea na halmashauri Kuu , tushirikiane kuhamasisha zoezi hili ili 
kupambana na ugonjwa huu ,ugonjwa upo ,tujihadhari "alisisitiza Gunini.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...