Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mahakama
kuu ya Tanzania imefutilia mbali kesi no 193 ya mwaka 2008 iliyokuwa
imefunguliwa na muwekezaji wa kiwanda cha chai Lupembe dhidi ya wakulima
wa chai waliyochini ya mwanvuli wa chama kikuu cha ushirika tarafa ya
Lupembe MVYULU kwa kufanya uvamizi wa kiwanda na kukiuka taratibu za
mkataba wa mauziano ya kiwanda.
Kesi
hiyo iliyolindima kwa zaidi ya miaka 14 tangu ifunguliwe huku kila
upande ukiamini kuwa sahihi kwa unachokiamini na kukisimamia na
kupelekea viongozi wakubwa wa serikali akiwemo waziri mkuu,waziri wa
kilimo na katibu mkuu kufika kwa nyakati tofauti kusuruhisha
mgogoro,Hatimae imefika mwisho baada ya september 24 mahakama kuu ya
jijini Dar es salaamu kutupilia mbali kesi hiyo na kisha kutamka MVYULU
kuwa mmiliki halali wa kiwanda hicho.
Akizungumza
na wananchi na viongozi kutoka kata zote za jimbo la Lupembe mbunge wa
jimbo hilo Edwin Swale amesema hakuna tena kesi dhidi ya Muwekezaji na
wananchi wa Lupembe kwa kuwa mahakama imeamuru kesi hiyo kufutwa baada
ya kuifatilia kwa zaidi ya miaka 17 na kwamba kilichobaki ni kukabidhiwa
tena wananchi baada ya uhakiki.
“Kesi
namba 94 ya mwaka ya mwaka 2016 ambayo ambayo ili lufaa iliyokuwa
mahakama ya Lufani ikihusisha wakulima wa chai Lupembe na muwekezaji
imekwisha na mahakamni hakuna tena ile kesi”alisema Swale
“Jamabo
la pili hukumu ya mahakama kuu iliyotamka watu wa Lupembe kulipa
mabilioni ya fedha ambayo ni hukumu ya kesi namba 193 ya mwaka 2008
imefutwa haipo tena na tuliyokubalina sasa kiwanda cha wananchi wa
Lupembe baada ya kufanyiwa ukaguzi mkubwa kinakabidhiwa rasmi kwa
wananchi wa tarafa ya Lupembe aliongeza Swale
Nae
Wlfred Swale ni mwenyekiti wa muungano wa vyama vya ushirika tarafa ya
Lupembe Mvyulu akiweka bayana mchakato wa kesi na msimamo wa wakulima wa
chai Lupembe anasema chanzo cha mgogoro wa umiliki wa kiwanda hicho ni
serikali kwasababu iliuza hisa za wakulima kwa muwekezaji wakati wao
ndiyo waliokinunua kwa mzungu aliejulikana kwa jina Wiliamson kwa
kukatwa fedha za majani
“Mgogoro
wa kiwanda kile una miaka 17 kutoka mwaka 2004 mpaka tarehe 24 ijumaa
ya mwezi wa 9 ndio uamuzi umefanyika,tulikwa tumeshindwa kesi tukaapeal
kwenye mahakama ya rufaa tumeendesha kwa milolongo mingi na kesi ilikuwa
kwasababu serikali imeuza hisa za wakulima 70 tukabakiwa na hisa
30”alisema Wilfred Swale
Ujio
wa taarifa za kurejeshwa kwa kiwanda cha Lupembe kwa wakulima wa chai
walio chini ya mwamvuli wa MVYULU kumepokelewa kwa hisia na wakazi wa
Lupembe ambapo mzee Gerson Mwavika na Elida Malekela wanasema walianza
kulisusa zao la chai kwasabau ya kunyang'anywa kiwanda chao walichokatwa
baba na mama zao fedha za majani ya chai na kahawa ili kukinunua kwa
mzngu.
“Tulikuwa
tunapambana kwasababu hata mimi ni mmoja kati ya wale ambao tulikuwa
tunatoa fedha kupitia chai kidogo,kahawa na pareto zilizokuwa zinakatwa
kwenye ushirika na ndio ushirika ulinunua kiwanda hiki kwa hiyo sisi
tulikuwa na haki”alisema Gerson Mwavika
“Tulichangia
fedha kutoka kwa baba zetu na sisi pia tulipoingia ushirika tulichangia
kwa hiyo kwa sasa tunahitaji mwekezaji ambaye anatuthamini
wakulima”alisema Elida Malekela.
Baadi ya wananchi wa Lupembe wakiwa wamebeba mabango ya pongeza kwa mbunge wao kwa ajili ya kuwapambania na kurejesha kiwanda hicho mikononi mwa wakulima.
Mbunge wa jimbo la Lupembe mkoani Njombe wakili Edwirn Swale akieleza
uamuzi wa mahakama dhidi ya kesi kwa wananchi wa tarafa ya Lupembe
mkoani Nyombe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...