Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali walioshiriki katika mkutano huo.
Mkurungenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akipokea cheti cha udhamini wa mkutano wa 53 wa Chama Cha Madaktari Tanzania (MAT) kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akizungumza wakati wa ufunguzi katika mkutano wa MAT jijini Mwanza.

SERIKALI imesema itakishirikisha Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO-19, kwa lengo la kutoa elimu zaidi nchini ya kujikinga na ugonjwa huo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Chama cha Madaktari Tanzania unaofanyika Jijini Mwanza.

“Wizara inatangaza rasmi MAT kuwa sehemu ya mapambano ya UVIKO-19, kuanzia sasa wataalamu wabobezi watashirikishwa katika majukumu ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huu,” amesema Mhandisi Gabriel.

Amsema Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeamua kuwashirikisha madaktari kwa kuwa wana utaalamu mkubwa wa masuala ya afya, lakini pia kuondoa upotoshaji unaofanywa na watu mbalimbali wasiokuwa na utaalamu.

Pia, Mhandisi Gabriel amesisitiza madaktari kuendelea kutoa elimu kwa jamii jinsi ya kijikinga na UVIKO-19 ili kuondoa hofu na maswali mbalimbali kuhusu chanjo ya UVIKO-19.

“Tumejitahidi kutoa elimu kuhusu umuhimu wa wananchi kuchanja na kuchukua tahadhari, elimu imesaidia, sasa tumeanza kuona mabadiliko, watu wanajitokeza kwa wingi kuchanja,” amesema Mhandisi Gabriel.

Katika mkutano huo, vile vile Mhandisi Gabriel amewataka madaktari kulinda taaluma yao kwa kusimamia maadili na kuchukua hatua kwa wale wanaokiuka maadili ya udaktari kwani wasipofanya hivyo, wananchi watakosa imani kwao.

Akizungumzia uboreshaji wa huduma za afya nchini, amesema Serikali itaendelea kuongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba sambamba na kujenga vituo vya afya kote nchini, ngazi ya wilaya, mikoa na hospitali za kanda kwa lengo la kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru ameishauri MAT kufanya mikutano katika ngazi ya wilaya na mikoa ili kuongeza uhai wa chama hicho.

Pia, amewataka madaktari nchini kufanya utafiti wa dawa za asili kama zinafaa kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa UVIKO-19. “Kama utafiti utabaini zinafaa, wataalamu waseme na kama hazifai waseme ni kwanini hazifai,”amesema Prof. Museru.

Naye Rais wa MAT, Dkt. Shadrack Mwaibambe ameiomba Serikali kuangalia upya gharama za kuhuisha leseni kwani gharama ya sasa TZS. 100,000 ni kubwa na kwamba inaweza kufikia hadi TZS. 400,000 endapo zikijumuishwa na gharama nyingine ndogo, ndogo.

Mkutano huo MAT, unafanyika kwa siku mbili jijini Mwanza ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa na kujadiliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...