Na Joseph Lyimo

BADO kwenye jamii zetu kuna watu wanaendekeza matukio ya kuwapiga wake zao ili kuwaonyesha kuwa wanawapenda na wengine huwaagiza wanyoe vipara kichwani ili wawapige vibao na kuingia ipasavyo vichwani.

Mkazi wa kata ya Gehandu, Mathayo Lohay amesema matukio ya ukatili mbalimbali wa wanawake wa eneo hilo ni jambo la kawaida na jamii haitaki mabadiliko kwenye hilo.

Lohay anasema kuna baadhi ya maeneo kama Gehandu, Bassotu na Dirma wanawake wananyolewa vipara ili wapigwe vibao kichwani na waume zao pindi wanapokosana kwenye ndoa zao.

“Wanaume wanawanyoa vipara wake zao na unakuta mtu mmoja ana wake watatu na kila mwezi kila mwanamke mmoja anapaswa kupigwa ili kuonyeshwa kuwa anapendwa,” amesema Lohay.

Anasema kutokana na hali hiyo ya kupigwa kuendelea kila wakati mwanamke hapaswi kupeleka suala hilo polisi au mahakamani kwani atatengwa kwa kuonekana kuwa unadharau mila na desturi zao.

“Mwanamke akifikisha suala hilo polisi tuu basi anasababisha kutengwa na jamii hasa wazee maarufu ndiyo wanashinikiza suala hilo,” amesema Lohay.Mwanamke mjane mkazi wa Dirma, Magdalena Jonas anasema yeye ni muhanga wa kunyang’anywa mali na ndugu wa marehemu mara baada ya mumewe kufariki dunia na kumuacha na watoto watatu.

Magdalena anasema hakuridhishwa kabisa kutokana na kunyang'anywa mali aliyokuwa nayo mume wake alipofariki dunia na kusababisha shemeji yake kumnyanyasa.“Mume wako akifariki dunia ndugu wa kiume wa mume wanakuja kukurithi na kisha wanakuja kuchukua mali ya familia," amesema.

Mkazi wa kata ya Endasak, Rose Dahay anakiri kuona wanawake wakifanyiwa ukatili wa kiuchumi kwa kunyimwa haki za kumiliki mali hata mwenza wake anapofariki na kushindwa kuhudumia familia.

“Serikali inapaswa kutoa elimu kwa wananchi wa eneo hili la Hanang’ kwani matukio ya ukatili wa kijinsia unapaswa kukomeshwa hasa kwa karne hii ya sasa,” amesema Dahay.Hata hivyo, Afisa wa ustawi wa jamii wa Wilaya ya Hanang’ Martha Sulle anasema matukio ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake kwenye eneo hilo yamekuwa yakitokea mara kwa mara.

Sulle amesema kwa mujibu wa taarifa walizonazo, wanawake 1,200 wamefanyika vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo vipigo kutoka kwa wenzawao na ukatili wa kimwili katika kipindi cha mwaka 2020 hadi mwaka 2021.

Amesema kesi nyingi za ukatili zinamalizwa kifamilia suala ambalo linasababisha kushamiri kwa vitendo vya ukatili kwenye wilaya hiyo ya Hanang’.“Inatosha kupinga maovu, inatosha kudai huyu ni ndugu yangu amemlawiti mtoto wa kaka yangu, au mume amempiga mke hadi kumvunja mkono na kunyamazia hayo inatosha sasa,” amesema Sulle.

Amesema matukio ya wanaume kuwapiga wake zao hadi kuwavunja mkono kisha kuwachinjia mbuzi au ng’ombe pindi wakikosana inabidi yafikie ukingoni na kumalizika kabisa.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...