Na Humphrey Shao, Michuzi Tv
Mbunge wa Busanda Mhandisi Mhe. Tumaini Magesa ameliomba Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) Kufikiria kuwekeza katika jimbo la Busanda kutokana namahitaji ya nyumba katika eneo hilo kutokana na kukua kwa kasi kwa mji huo.
Magesa amesema hayo leo mara baada ya kutembelea banda la NHC katika Maonesho ya 4 ya Teknolojia na Uwekezaji Sekta ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Bombambili-EPZ Mkoani Geita.
''Nalipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa kazi nzuri inayofanya katika utekelezaji wa miradi yake iliyotapakaa sehemu mbalimbali nchini, na kuikaribisha NHC kujenga nyumba za Makazi eneo la Busanda kwani wahitaji ni wengi na hazitakawia kuisha".Amesema Magesa.
alisisitiza kuwa wao wakazi wa Busanda ndio wachimbaji madini na wao ndo wenye dhahabu kwani kama shirika likiweza kuwekeza busanda kamwe alitojutia kwani nyumba zitajengwa na kuuzw akwa haraka haraka.
Afisa Mauzo Mwandamizi kutoka shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Daniel Kure akizungumza jambo na Mbunge wa Busanda Tumaini Magesa juu ya miradi mbalimbali ya NHC,
,
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...