Na Khadija Seif, Michuzi TV

MSANII wa muziki wa Mduara Juma  Kivurande amesema yeye ni shabiki mkubwa wa mwanamuziki Kassim Mganga na amefurahi kupata nafasi ya kumshirikisha mkali huyo wa mwanamuziki mduara.

Akizungumza leo Septemba 22,21  Kivurande amesema yeye ni shabiki mkubwa wa Kassim  tangu enzi za Awena, hivyo alikua na shahuku siku moja apate nafasi ya kutoa ngoma pamoja naye.

"Kupitia Meneja wangu HK alifanya mipangilio yote na kunikutanisha naye na hatimaye tukaingia studio tukakamilisha wimbo wangu unaokwenda kwa jina la "Namcheza Mwari".

Aidha ameeleza ugumu alioupata wakati anatengeneza wimbo huo akiwa pamoja na Kassim Mganga."Kutokana na shahuku pamoja na ile hofu nikajikuta kama siamini kama leo kweli tunatengeneza wimbo wetu ambao mategemeo makubwa kuwa mashabiki zetu wataupokea.

"Sababu na amini uwezo wa Kassim kwenye Muziki wa Mduara na ametoa baadhi ya vibao kama Somo na Mwari, Harusi yangu na vingine vingi ambavyo hadi leo vimekua vikiburudisha kwenye sherehe mbalimbali".

Kwa upande wake Kassim Mganga a.k.a Gwiji amesema kushirikishwa kwenye wimbo huo imekuwa ni nafasi nzuri ya kushirikiana wanamuziki kutoka Tanga kuonesha umoja wao.

"Hadimu mno kuona wasanii wanaofanya muziki unaofanana na wanaotoka sehemu moja kushirikiana kwenye kazi za muziki.Nitoe tu hofu kwa nashabiki zetu kuwa mimi nafatilia muziki wa mdogo wangu Kivurande na hata alipohitaji tufanye ngoma sikuona haja ya kukataa wala kuchelewesha ili tuwape mashabiki zetu kitu kizuri,"amesema.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...