Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Bondia nyota nchini Salimu Jengo atapanda ulingoni Oktoba 13 kuwania mkanda wa Shirikisho la ngumi za kulipwa Afrika (ABU) dhidi ya bondia Hannock Phiri kutoka Malawi.
Pambano hilo la raundi 12 la uzito wa Super Light limeandaliwa na kampuni za Swahiliflix na Win Win Sports Promotion la uzito wa super light la raundi 12 litafanyika kwenye ukumbi wa Mtana uliopo kwenye jengo la Millenium Tower 2, Makumbusho, jijini.
Mkurugenzi wa masoko wa Swahiliflix Amos Chibaya alisema kuwa mkanda huo upo wazi na kuamua kumpa nafasi Jengo kuwania mkanda.
Chibaya alisema kuwa pambano hilo litaonyeshwa ‘live’ na mtandao wao wa Swahiliflix app ambayo inapatikana Google Play Store na vile vile kupitia Apple TV.
Alisema kuwa mbali ya pambano hilo, pia kutakuwa na ‘vita’ ya pambano la marudiano kati ya bondia Shawn Miller kutoka Marekani na Shaaban Jongo la uzito wa cruiser la raundi nane.
Alifafanua kuwa Miller ameomba kurudiana na Jongo baada ya kupoteza kwa TKO.
“Swahiliflix inayofuraha kuingia katika ngumi za kulipwa nchini kwa kushirikiana na wadau wengine kama Win Win Sports Promotion, Urban soul, Global Boxing Stars na Onomo hotel. Tunatarajia kuona mapambano makali nay a kusisimua kwani kila bondia amepania kushinda,” alisema Chibaya.
Alisema kuwa mbali ya kuandaa mapambano, kampuni yao pia itasaidia kutoa ushauri ili kuendeleza vipaji vya ngumi za kulipwa kimataifa.
Alifafanua kuwa wamepania kufanya mambo makubwa katika ngumi za kulipwa hapa nchini kupitia mtandao wao wa kimataifa wa Swahiliflix.
Mbali ya mapambano hayo mawili, pia kutakuwa na pambano kali kati ya bondia kutoka Kenya Ryton Okwiri ambaye atapambana na bondia wa Uganda John Serunjogi ambapo bondia Joseph Sinkala atazichapa na Hamis Maya na Alex Kachelewa atapimana ubavu na Shadrack Ignas.
Pia kutakuwa na pambano la bondia nyota wa Congo Brazaville Adi Ndembo dhidi ya bondia ambaye atatangazwa hapo baadaye.
Kwa upande wake, Jengo alisema kuwa amejiandaa vyema kupambana na Phiri ambaye alikuja hapa nchini na kumchapa bondia Hannock Phiri kutwaa ubingwa wa WBF Afrika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...