Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Mradi
wa mabasi ya mwendokasi umeongeza ruti za safari za mabasi hayo na sasa
umeanza kutoa huduma zake hadi stendi ya Kibaha na mengine yakifika
hospital ya MUHAS Mloganzila.
Kufuatia kuongezwa kwa ruti hizo
wakazi wa Kibaha na maeneo jirani wamepongeza Serikali kwa kukomboa
wanyonge wakiwemo wanafunzi kwa kusogeza huduma ya uhakika ya usafiri.
Katika vituo vya Mailmoja ,Kibamba , Mloganzila wameonekana watoa huduma ambapo wananchi wamejitokeza kwa wingi.
Mkazi
wa Mailmoja Salehe Issa alieleza ,Ni rahisi kwao kutoka Kibaha wakifika
hapo wanaunganisha usafiri wa mabasi hayo katika njia kuu za Kimara na
Kwingine hali ambayo imesaidia kwa kiasi kikubwa katika utoaji nauli na
muda.
"Tunaushukuru uongozi wa mabasi ya mwendokasi (UDART) kwa
kutuleteaa usafiri kutokeaKimara hadi Maili Moja Kibaha"Tulikuwa
tukipata usumbufu kutokea Mbezi kuja hapa kwa kuzuiliwa tusipande mabasi
madogo hadi abiria wa mbali wapande kwanza"
Nae Ramadhan Kazembe
alieleza ,Mbezi tulikuwa haturuhusiwi kupanda hadi abiria kuanzia Picha
ya Ndege hadi Mlandizi wakae kwenye viti na wakishakaa abiria wa Maili
Moja ndiyo wapande.
"Hizi coaster za kutuambia mpaka wajaze
halafu sisi wa Maili Moja tusimame walikuwa kweli hawatutendei haki bora
tutapumzika na manyanyaso ," alisema Ramadhan Kazembe.
Mkazi
mwingine, Tumaini Thonya alifafanua, ana amani kwani jamaa wananyanyasa
sana kauli mbovu ,ubabe hawajui mlemavu, mzee, mjamzito wala wenye
vichanga .
Thonya alibainisha, daladala hasa kutoka kule kuja
huku wale wanaosema hawapakii Maili Moja Kibaha kimara 650 na Kariakoo
1,300 sasa wamepata kiboko yao.
Kwa upande wake Mohamed Lipwai
alisema kuwa usafiri huo ni wa uhakika na ni furaha maana waliteseka
kwenye daladala ilikuwa ikifika jioni hawataki kupakia abiria wa Maili
Moja wakidai nauli yao ya shilingi 500 ni ndogo.
Amina Ally
alisema ,hata wangesema 3,000 kuliko panda shuka panda shuka mbona
walikuwa wakipanda panda sana noah kutoka Kariakoo hadi Mbezi 5,000 na
Kimara bajaji kwa 2,000 hivyo kwao ni furaha na wanawapongeza kwa hatua
hiyo.
Mradi huo ulioanza kazi rasmi kwa majaribio mwaka 2016 ,
umesaidia kupunguza adha ya usafiri kwa wakazi hususani waishio Kimara
na Mbezi licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo uchache wa
mabasi.
Ruti zilizokuwepo ni pamoja na Mbezi-Kivukoni,
Mbezi-Gerezani, Kimara-Kivukoni, Kimara-Gerezani, Kimara-Morocco.
Nyingine ni Morocco-Gerezani, Morocco-Kivukoni ,Muhimbili-Gerezani na
Kawe.
Wakati unaanza ulikuwa na mabasi 140 na unaendeshwa na kampuni binafsi ya Udart huku DART ikibaki kama msimamizi wa miundombinu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...