NA WAMJW- KIBITI, PWANI.

MKUU wa Wilaya ya Kibiti Kanali. Ahmed Abasi Ahmed ametoa wito kwa wananchi kuachana na Imani potofu zinazotolewa na watu wasio na nia njema kwa wananchi na kuwataka kuwasikiliza zaidi Wataalamu wa afya na viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19.

Ameyasema hayo leo waati akifungua kikao cha kamati ya Afya ya msingi ya Wilaya Kibiti, chenye lengo la kuhamasisha wananchi kupata Chanjo ya UVIKO-19 kupitia kampeni shirikishi na harakishi inayoongozwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na OR TAMISEMI.

"Nichukue nafasi hii kuwasisitiza wananchi kuachana na Imani potofu, wawasikilize Wataalamu wa huduma za Afya lakini pia wawasikilize viongozi wilio na dhamana ya kutuongoza katika mapambano haya makubwa ya UVIKO-19 tulionayo" amesema Kanali. Ahmed.

Natambua Serikali imewekeza nguvu kubwa katikati mapambano dhidi ya ugonjwa huu wa UVIKO-19, na sisi kama Wadau wa vita hii, tuunge mkono jitihada hizi za Serikali ili kushinda dhidi ya vita hii. Alisisitiza.

Aidha, Amesema kuwa, Shirika la Afya Duniani na Wataalamu wa ndani tayari wamethibitisha Chanjo ni salama, haina madhara, hivyo kuwataka kwasikiliza watoa mafunzo kwa makini ili kwenda kuwaelimisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupata Chanjo ili wajikinge dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19.

"Shirika la Afya Duniani na Wataalamu wetu wameshatuhakikishia Chanjo hii ni salama, haina madhara, hivyo niwaombe tuwasikilize kwa makini Wataalamu wetu waliokuja kutupa mafunzo na tutayojifunza twende tukawaelimishe wananchi wetu ili wajutikeze kwa wingi kupata Chanjo ili wajikinge dhidi ya ugonjwa huo." Amesema.

Mbali na hayo, amesema kuwa, Wilaya hiyo ilianza kuwa na vituo vitatu vya kuchanja baadae kuongezeka mpaka vituo vitano na kuweka wazi kuwa, mpaka sasa vimeongezeka na kufikia vituo zaidi ya hamsini na nne (54), ikiwa ni jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Afya kuwakinga wananchi dhidi ya UVIKO-19.

Hata hivyo amesema kuwa, pamoja na uwepo wa vituo hivyo bado kasi ya watu kujitokeza kuchanja sio kubwa, hivyo kuwataka wajumbe katika kikao hicho kufuatilia kwa makini mafunzo yaliyokuwa yakitolewa ili kuwa na uelewa wa kutosha juu ya umuhimu wa chanjo na kuweza kuwashawishi wananchi kujikinga dhidi ya UVIKO-19 kupitia afua ya Chanjo


 


 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...