Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzanoa leo imetimiza ahadi zake zilizotolewa na Rais wa Samiah Suluhu Hassan kwa kupeleka vifaa tiba katika Hospitali ya Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani.
Vifaa hivyo vina thamani ya Shilingi Milioni 480 ikiwemo mashine ya Kupiga picha za Mionzi yaani X-Ray, Jokofu la kuhifadhia maiti, mashine za kupimia damu na vifaa mbalimbali.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa kwa vifaa hivyo Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ameishukuru Serikali kwa kutekeleza ahadi hii ndani ya muda wa wiki tatu toka kutolewa kwa ahadi.
Wananchi wa Kata hiyo wakiongozwa na wakina mama ambao walikuwa ipokea wameshangilia na huku wazee wakimuombea Mungu amlinde Rais wa nchi yetu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...