Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amewahakikishia wakulima wa zao la korosho kutokatwa fedha za pembejeo sababu tayari serikali imetoa Bilioni 60 kwaajili ya pembejeo.
Kauli hiyo ameitoa jana tarehe 17 Septemba, 2021 mkoani Mtwara katika eneo la mnazi mmoja ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Sekretarieti ya CCM Taifa katika Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Njombe.
Katibu Mkuu amefafanua kuwa, Miaka ya nyuma serikali ilikuwa ikitoa bilioni 50 kila msimu ambapo wakulima walikuwa wakikatwa fedha hizo pindi wanapoenda kuuza Korosho zao.
Amesema, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha hizo shilingi bilioni 60 kwa ajili ya pembejeo mwanzo wa msimu ili kuwasaidia wakulima kupata faida kubwa, na hakuna mkulima atakayekatwa fedha hizo kama ilivyokuwa awali.
Wakati huo huo, Katibu Mkuu ameeleza kuwa, Mwaka huu Rais Samia ameelekeza Korosho zote kupakiwa katika bandari ya Mtwara na sio ya Dar es Salaam kwaajili ya kusafirishwa, kwani bandari hiyo imegharimu shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya upanuzi ili kuiongozea uwezo na kuwanufaisha wakulima wa mikoa ya kusini.
Home
SIASA
RAIS SAMIA AMETOA SHILINGI BILIONI 60 KWA AJILI YA WAKULIMA WA KOROSHO NCHINI- KATIBU MKUU CCM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...