Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila amefanya ziara Kata ya Kiloleli Wilayani Busega kwaajili ya kusikiliza kero za wananchi wa Kata hiyo siku ya tarehe 24 Septemba 2021, na kuwatoa hofu juu ya kero na changamoto zinazowakabili.



Mkutano huo uliochukua takribani masaa matatu umewapa fursa wananchi wa Kata ya Kiloleli kueleza kero na changamoto zinazowakabili. Miongoni mwa kero zilizowasilishwa na wananchi hao ni pamoja na changamoto za upatikanaji wa maji baadhi ya maeneo, changamoto ya barabara, umeme, maji na uvamizi wa wanyama wakiwemo Viboko na Tembo.

Pamoja na wananchi hao kueleza kero zao mbele ya Mhe. Kafulila ambapo aliwataka wataalam alioambatana nao kutoka Wilayani Busega kutoa maelezo ya changamoto zilizowasilishwa na wananchi na zile ambazo hazikuwa na maelezo ya papo hapo aliwaeleza wananchi wa Kata hiyo kwamba ataendelea kuzifuatilia kwaajili ya kuzipatia utatuzi.

Mbali na hayo, Mhe. Kafulila amewatoa hofu wananchi wa Kiloleli kwa kuwaeleza kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ina azma na malengo ya kuhakikisha inasimamia Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ili kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Aidha, Mhe. Kafulila amesema kwamba kwa kudhiirisha hilo, tayari Serikali ya Awamu ya Sita imeweza kuleta fedha kwaajili ya Miradi mbalimbali ikiwemo Miradi ya Elimu, Afya, Maji na Barabara. “Mkoa wetu umepokea kiasi cha Tshs Bilioni 12 kwaajili ya ujenzi wa Barabara Vijijini, zaidi ya Tshs Bilioni 8.8 kwaajili ya Miradi ya Maji, na miardi mingine mingi”, aliongeza Kafulila.

Wananchi wa Kata hiyo pamoja na kueleza kero na changamoto zao pia wameiomba Serikali kujenga chuo cha ufundi Mkoa wa Simiyu na Wilayani Busega ili kuwawezesha vijana ambao hawapati nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari na elimu ya juu kujinga na masomo ya ufundi. Akieleza kwa kina juu ya suala hilo Mhe. Kafulila amesema katika Mkoa wa Simiyu hakuna vyuo vya ufundi ambavyo vipo chini ya VETA, lakini juhudi tayari zimeanza hivyo taratibu zote zikikamilika Mkoa utapata chuo cha ufundi VETA ili kuwawezesha vijana kupata fursa ya masomo ya ufundi, hivyo wananchi wawe na subira. Mhe. Kafulila anaendelea na Utaratibu wake wa kusikiliza kero za wananchi maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Simiyu, na hii ni zaidi ya mara tatu kufanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi Wilayani Busega.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...