Katika kuunga mkono agenda ya kusaidia matibabu ya Fistula kwa kina mama wasio na uwezo, wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania hii leo wameungana na maelfu ya watanzania wengine akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kushiriki mbio za Hisani za NMB Marathon zilizokuwa na kauli mbiu 'Mwendo wa Upendo,' zikilenga kukusanya kiasi cha Sh Bilioni 1 ili kufanikisha mpango huo.
Mbali na kushiriki mbio hizo Benki hiyo pia ilitoa mchango wa fedha kiasi cha Sh Mil 10 kwa waandaaji wa mbio hizo ili kuunga mkono jitihada hizo.
Wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wakijipongeza na medali zao baada ya kushiriki mbio za Hisani za NMB Marathon zilizokuwa na kauli mbiu 'Mwendo wa Upendo,' zikilenga kukusanya kiasi cha Sh Bilioni 1 ili kufanikisha mpango wa matibabu ya Fistula kwa kina mama wasio na uwezo mapema hii leo. Mbali na kushiriki mbio hizo Benki hiyo pia ilitoa mchango wa fedha kiasi cha Sh Mil 10 kwa waandaaji wa mbio hizo ili kuunga mkono jitihada hizo
Tupo tayari kwa mbio! Ndivyo wanavyoonekana wakisema wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania walipojitokeza kushiriki mbio za Hisani za NMB Marathon zilizokuwa na kauli mbiu 'Mwendo wa Upendo,' zikilenga kukusanya kiasi cha Sh Bilioni 1 ili kufanikisha mpango wa matibabu ya Fistula kwa kina mama wasio na uwezo mapema hii leo. Mbali na kushiriki mbio hizo Benki hiyo pia ilitoa mchango wa fedha kiasi cha Sh Mil 10 kwa waandaaji wa mbio hizo ili kuunga mkono jitihada hizo
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wakishiriki mbio hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...