Na Muhidin Amri, Songea

SERIKALI imesitisha  kazi ya ununuzi wa mahindi katika kituo Kikuu cha Ruhuwiko katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, iliyokuwa inafanywa na wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa Chakula(NFRA) kanda ya Songea.

Serikali imefikia  hatua hiyo baada ya kubaini na kujiridhisha kuwa, mahindi mengi yanayopelekwa  katika kituo  hicho ni  ya wafanyabiashara  na sio wakulima ambao wamelengwa kunufaika na bei  ya Sh. 500 kwa kilo moja.

Uamuzi huo umetolewa jana na  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge,aliyeambatana na Waziri wa kilimo Profesa Adolf Mkenda wakati akikagua kazi ya ununuzi wa mahindi unaofanywa na wakala waTaifa wa Uhifadhi wa chakula(NFRA)kanda ya Songea  katika wilaya ya Songea na Mbinga.

Badala yake amesema,kituo hicho kitumike kupokea mahindi  ya wakulima yanayonunuliwa kutoka katika vituo vingine vya vijijini.

 “serikali haiwachukii na wala haina ugomvi na  wafanya biashara isipokuwa imefikia uamuzi huo ili kuwafikia,kuwalinda na kuwasaidia wakulima wasiokuwa na uwezo wa kupeleka mahindi nje ya nchi ili fedha watakazopata ziweze ziendelee kuongeza uzalishaji kwa msimu ujao”amesema.

Hata hivyo,ameruhusu mahindi yaliyopo katika kituo hicho ambayo yamekaa  kwa muda mrefu na wamiliki wake wameorodheshwa na NFRA yanunuliwe na ambayo  yameletwa baada ya apo  yaondolewa  katika eneo hilo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa amesema,  katika msimu wa kilimo 2020/2021 mkoa huo umezalishaji tani  milioni 1,623,510 ya mazao  ya chakula, biashara na bustani kati ya lengo la kuzalisha tani 1.785,500 sawa na asilimia 91.

Amesema, kati ya hayo uzalishaji wa mazao ya chakula nit ani 1,384,705,mazao ya biashara tani 67,772 na mazao ya bustani zilizalishwa jumla ya tani 158,795.

Kwa mujibu wake, mkoa wa Ruvuma hadi sasa una chakula cha kutosha  nakinachoendelea kutumika kilizalishwa katika msimu 2020/2021ambapo jumla ya tani 1,384,705 zilizalishwa.

Hata hivyo amesema, mahitaji ya chakula kwa wakazi wa mkoa huo ni tani
470,000 na kubakiwa na ziada ya tani 914,705 ambayo imeendelea kuuzwa
kwa ajili ya kuwapatia wakulima kipato.

Aidha amesema, msimu 2020/2021 mahindi yamenunuliwa kupitia soko la
huria na taasisi za Serikali  ambazo ni wakala wa Taifa wa Uhifadhi wa
chakula(NFRA) na Bodi ya mazao mchanganyiko(CPB).

Amesema, katika awamu ya kwanza NFRA  imenunua jumla ya tani  60,000
kati ya lengo la kununua tani 32,000 kwa wastani wa bei ya Sh.500 kwa
kilo moja kwenye kituo kikuu na Sh.470 kwenye vituo vilivyoko vijijini
 na katika awamu ya pili NFRA kanda ya Songea imepewa lengo la kununua
tani 35,000 kwa bei ya Sh.500 kwa kilo kwenye vituo vyote.

Kwa upande wake, Waziri wa kilimo Profesa Adolf Mkenda amemshukuru
Rais Samiha Suluhu Hassan kwa kuongeza  kiasi cha Sh. Bilioni 50 ili
kununua mahindi ya wakulima ambapo kwa kanda ya Songea wameongezewa
tani 35,000  kutoka tani 6,000 za awali.

Amesema, dhamira ya Rais Samiha ni kuona fedha hizo zinawafikia moja
kwa moja wakulima na sio wafanyabiashara ambapo amempongeza Mkuu wa
mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge kwa usimamizi mzuri wa
ununuzi wa mahindi.

Amesema, bei ya Sh.500 kwa kilo ni ruzuku iliyotolewa na Serikali ili
kila mkulima aweze kupata bei hiyo badala ya kuwanufaisha watu
wachache wanaonunua mahindi  ya wakulima kwa bei ndogo na kwenda kuuza
kwa NFRA.

Profesa Mkenda amefafanua kuwa,utaratibu wa sasa kila mkulima atapata
nafasi ya kuuza gunia 100 na sio vinginevyo na kueleza kuwa,wale
watakaokosa nafasi hiyo wanaweza kuuza mahindi kwa Bodi ya mazao
mchanganyiko(CPB)ambayo itaanza shughuli zake hivi karibuni.

 Waziri wa kilimo Profesa Adolf Mkenda katikati akizungumza jana na baadhi ya wakulima wa mahindi katika kijiji cha Mgazini kata ya Kilagano Halmashauri ya wilaya Songea mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake ya kuangalia kazi ya ununuzi wa zao hilo unaofanywa na wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula NFRA kanda ya Songea,kushoto Mkuu wa mkoawa Ruvuma Brigadia Jenerali Wilbert Ibuge na kulia Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema. Picha na Muhidin Amri.

Mkuu wa mkoa wa Ruvumhindi waliopeleka mahindi yao katika kituo cha kuuzia mahindi Mgazini kata ya Kilagano wilaya ya Songea ambapo amepiga marufuku wafanyabiashara kuuza mahindi yao kwa wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula NFRA badala yake ameagiza wakulima wadogo ndiyo watakaouza mahindi katika vituo vilivyotengwa,kulia Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema.

 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...